May 12, 2017

NDEGE YA KUWASAFIRISHA MAJERUHI WA LUCKY VINCENT KUWASILI LEO NCHINIArusha. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema wamekamilisha  safari ya kuwapeleka Marekani majeruhi watatu wa ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha.
Akizungumza leo (Alhamisi) katika ofisi ya mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Nyalandu amesema ndege maalumu ya kuwabeba majeruhi hao  imetolewa na Shirika la Samaritan Fund la nchini Marekani ambayo itawasili LEO
Nyalandu amesema rubani anatarajiwa kuwasili jijini Arusha JANA akitokea Nairobi nchini Kenya na iwapo kila kitu kitakamilika safari itakuwa Jumamosi.
"Watakaoondoka ni abiria wanane, ambao ni majeruhi na wazazi wao, muuguzi mmoja na daktari mmoja. Hati za kusafiria ziko tayari, kinachosubiriwa ni viza," amesema Nyalandu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE