May 18, 2017

MTOTO DOREEN MAJERUHI WA LUCKY VINCENT AINGIZWA KWENYE UPASUAJI MUDA HUU


Mwanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent, Doreen Mshana akiwa wodini akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mercy iliyopo jijini Sioux.

 Mtoto Doreen Mshana, ameingia kwenye chumba cha upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo asubuhi hii nchini Marekani anakotibiwa huku madaktari wakiwataka Watanzania wamuombee.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu(CCM) ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa madaktari  wanaingia kwenye chumba cha upasuaji  huo asubuhi hii.
Upasuaji huo  unatajwa kuwa ni mkubwa na mgumu.
“Taifa na kila mtu tumuombee mtoto wa Doreen. Anaenda kufanyiwa upasuaji mgumu wa uti wa mgongo.” umesema ujumbe wa madaktari hao aliotumiwa Nyalandu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE