May 24, 2017

MSANII DULLA MAKABILA MZEE WA SINGELI ' UNATOA HUTOI 'AFIKISHWA POLISI IRINGA

Msanii Dulla Makabila 


                                                         Na MatukiodaimaBlog
 MSANII maarufu wa Singeli anayevuma kwa  wimbo  wake wa ' UNATOA HUTOI' Dulla Makabila ameonjeshwa  joto la jiwe  mkoani Iringa  baada ya  kuchungulia hababusu  kwa kushindwa kufanya show Miss Chuo  kikuu Iringa .

Msanii  huyo  ambae  alilipwa  sehemu ya  fedha za show  hiyo iliyofanyika  ijumaa wiki  iliyopita  kwenye  ukumbi wa St Dominic kwa ajili ya  kumsaka mlimbwende  wa chuo kikuu cha Iringa zamani  Tumaini ,alishindwa  kabisa  kufanya show hadi  onyesho  hilo linamalizika majira ya saa 7  za usiku hakuweza  kutokea  ukumbini .

Mratibu  wa kampuni ya FNL ambao  ndio  walioandaa onyesho hilo Cosmas Kishamawe alimweleza  mwandishi  wa matukiodaimablog  kuwa baada ya  msanii  huyo kushindwa  kutokea  ukumbini kama mkabata  wake  ulivyoeleza alilazimika kwenda  kituo  cha polisi kwa ajili ya  kufungua kesi dhidi ya msanii  huyo .

Alisema wakati  wote  akiwa ukumbini hapo  mashabiki  waliofika ukumbini hapo  walionyesha  kuja juu kutaka msanii  huyo kupanda jukwaani kama walivyoelezwa kwenye matangazo ila kwa kuwa msanii  huyo alikuwa hajafika mkoani Iringa  waliishia kuwaomba  radhi  wateja wao.

" Kati ya  onyesho ambalo  tulilifanya kwa roho  juu na tukisubiri lolote  kutoka kwa mashabiki ni  hili maana wateja wetu  walikuja juu kutaka msanii  huyo apande  jukwaani  ila  muda  wote  tukimpigia simu anadanganya kuwa  yupo Ipogolo anapandisha  kuja mjini  toka majira ya saa moja  tunampigia anadanganya ...kweli alituharibia  sana"

Alisema  kuwa mida ya saa 7 kwenda  saa 8  usiku ndipo msanii  huyo alipiga simu  kuwa amefika mjini Iringa anahitaji kupokelewa ili kufika ukumbini kwa ajili ya show hiyo.

Mratibu  huyo alisema kutokana na muda wa  kuendelea na onyesho  hilo kuwa umemalizika aliamua kumchukua na kumpeleka  moja kati ya club  maarufu mjini hapa ili  apumzike japo mwenyewe Makabila aliomba  kupanda  jukwaani  kufanya onyesho la bure kwa ajili ya  kujitangaza .

" Wakati akiwa jukwaani akiburudisha  ndipo  mimi nilitumia  muda  huo kukimbia polisi na kuja nao kumkamata na kumpeleka Polisi ambako  alikaa hadi saa 9 Alfajiri na kulazimika  kurejesha  sehemu ya  pesa  alizolipwa na nyingine  kuandikishana  kuwa akirejea  Dar es Salaam atazituma kutokana na kuvunja mkataba wake .

Mtandao  huu wa matukiodaima ulimtafuta  bila  ushirikiano msanii  huyo kwa njia ya simu  huku  akiahidi   kulizungumzia  suala hilo baada ya dakika chache  ila kila akipigiwa aliishia kukata  simu pasipo  kuongea  chochote .

Soma  habari  hii ndani ya  gazeti la  Risasi  leo  jumatano May 24/2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE