May 25, 2017

MKOA WA IRINGA WAFANIKISHA UANDIKISHAJI DARASA LA KWANZA

Mwalimu  Herry  Lukuvi akikabidhiwa  zawadi  na mwakilishi wa mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza ,mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam  baada ya shule  yake  ya  sekondari  kufanya  vizuri  kwa  upande wa shule za  serikali
Viongozi mbali  mbali  akiwemo  Daud  Yassin kulia  wakiwa katika kilele  cha kusoma

wakuu  wa idara na watumishi wa Halmashauri na  mkoa wa  Iringa  wakiwa  katika kilele  cha kusoma mkoa  wa Iringa
Wanafunzi wa shule  mbali mbali  wakiwa kwenye uwanja wa  Mashujaa katika kilele  cha kusoma


Afisa  elimu  msingi  wilaya ya  Kilolo Allos Maira  kushoto  akitoa  taarifa kwa mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri  Wiliam kulia  wakati wa kilele cha kusoma ,katikati ni katibu  tawala  mkoa Wamoja Ayubu

Afisa  elimu  msingi  wilaya ya  Kilolo Allos Maira akifafanua jambo wakati mgeni  rasmi alipotembelea  banda la maonyesho ya  elimu Kilolo
Mwalimu  wa  kitengo maalum Kilolo  akitoa maelezo kwa mgeni  rasmi
Wanafunzi  wenye mahitaji maalum  wakionyesha uwezo wao katika kuhesabu
Mwanafunzi  wa darasa  la  saba  shule ya msingi  Luganga  Kilolo Benjamin Kadege  akionyesha  uwezo  wake katika hesabu
Viongozi  mbali mbali wakimtazama mwanafunzi Gradnes  Magoha  wa darasa la  la shule  Msingi Kilolo B
Kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa Richard  Mfugale akisoma taarifa ya elimu mkoa kwenye  kilele  cha Kusoma
Mwalimu  wa shule  ya Msingi Upendo  Mafinga KIssa  Mwassanga akicheza  na wanafunzi  wake ngoma  asili ya Msele kutoka mkoa  wa Lindi wakati  wa kilele  cha kusoma mjini Mafinga
Katibu  tawala  wa  mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu  akitoa  pongezi kwa  shule zilizofanya  vizuri  katika mitihani mbali mbali
Mwanafunzi  mwenye mahitaji maalum kutoka  shule ya msingi Makalala Mufindi Edina Kavindi  akipewa  zawadi 
viongozi wa mji Mafinga  wakifurahia  zawadi  baada ya  kuwa  Halmashauri  bora  kimkoa kufanya  vizuri katika masomo
madiwani  wakifuatilia  hotuba ya mgeni rasmi
Mwakilishi  wa mkuu wa  mkoa wa Iringa  Jamhuri Wiliam akiwahotubia  wananchi 
Mwalimu wa  shule maalum ya Makalala  Mufindi Clara  Mbawala  akiwa na motto mwenye ulemavu wa  ngozi Edna Kavindi aliyepata  zawadi  kwa  kufanya vema  katika masomo  yake .


Na MatukiodaimaBlog
MKOA  wa  Iringa  umefanikiwa  kuandikisha  wanafunzi wa  darasa  la kwanza 39,233 kati  yao  wavulana wakiwa  ni 17,443  na  wasichana ni 21,790  sawa na asilimia 110 ya  lengo la kuandikisha  wanafunzi 35,538 ambapo  uandikishaji  huo ni ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na uandikishaji wa mwaka 2016.


Akisoma  taarifa ya  hali ya  elimu  mkoa wa Iringa   leo wakati wa kilele  cha Kusoma   kilichofanyia kwenye  uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga kwa  mkoa wa Iringa ,kaimu  afisa  elimu  mkoa  wa  Iringa Richard Mfugale alisema  kuwa  mwaka 2016 mkoa  wa Iringa  uliandikisha  wanafunzi wa darasa la kwanza  35,855 wavulana  wakiwa ni  18,106 na  wasichana  17,749  na  kuwa ongezeko  kubwa la  wanafunzi kuandikishwa mwaka huu limechangiwa na  mpango wa  serikali ya awamu ya tano  wa  elimu bila malipo.
Alisema katika  uandikishaji  huo mwaka  huu 2017  Manispaa ya  Iringa  iliandikisha  wanafunzi 4,494,  halmashauri ya  Iringa iliandikisha wanafunzi  9,813, wilaya ya  Kilolo iliandikisha  wanafunzi  8,012, Mufindi  wanafunzi 14,296, na Mafinga  mji iliandikisha wanafunzi  39,233.
Pia alisema  mkoa  wa  una  shule  moja ya elimu  maalum  na vitengo 9 na kufanya  jumla ya wanafunzi 585 wa elimu maalum msingi ,kati  ya hao wavulana ni 316 na  wasichana ni 269 wakati  elimu maalum ya sekondari  haina  shule ya elimu maalum bali ina vitengo  vitatu vyenye jumla ya wanafunzi 155 kati yao  wavulana ni 89 na wasichana 66.
Mfugale  alisema kuwa  mkoa huo una jumla ya walimu wa elimu maalum 138 wanaume 63 na wanawake 75 na kuwa utoaji wa elimu maalum  katika mkoa umekuwa  ukitolewa  kwa mifumo miwili  mfumo wa kitengo (intergration ) na mfumo wa jumuishi  (inclusive system) lengo la  kuwapa elimu wanafunzi  wenye mahitaji maalum ili kuwajengea  maarifa ,stadi na mielekeo ya kuwawezesha kushiriki vema katika maendeleo ya sekta kadhaa wa kadha  kama vile  elimu ,afya, na ajira .
Kuhusu  elimu ya watu  wazima  nje na elimu ya nje ya mfumo rasmi alisema kuwa  uendeshaji wa programu  za elimu ya watu  wazima na elimu ya nje ya mfumo rasmi  imeendelea  kutolewa katika vituo vya MEMKWA 18 vyenye jumla ya  wanafunzi 338 kati yao wavulana ni 205 na wasichana ni 133 pia  kuna  jumla  ya vituo 73 vya MUKEJA  vinavyoendesha programu mbali mbali  .
" Mkoa  wa Iringa  una programu ya elimu changamani baada ya  elimu ya msingi  ambapo  kuna jumla ya  vituo  vilivyopo kwenye Halmashauri mbili Iringa na Mufindi .....mkoa  pia  una  kituo   cha taasisi ya elimu ya watu  wazima chenye jumla ya wanafunzi 367 wanaume 148 na wanawake 219"
Hata  hivyo  Mfugale  alisema mkoa una jumla ya vyuo  vikuu  vitano na taasisi  za elimu mbili na kutaja  vyuo  hivyo kuwa ni chuo kikuu cha Ruaha (RUCO) , chuo kikuu cha Iringa (UoI), chuo  kikuu  kishiriki  cha Mkwawa (MUCE) ,chuo  kikuu Huria cha Tanzania ( OUT) na chuo kikuu  kishiriki  cha ushirika  Moshi  pamoja na taasisi ya elimu ya  watu  wazima na  chuo  cha VETA .

Pia  alisema kuhusu  ufaulu  mkoa wa Iringa  umeendelea  kufanya  vizuri kwa kupandisha  ufaulu  kutoka asilimia 72 mwaka  2014  hadi  kufikia asilimia 89.2 kwa matokeo ya kidato  cha  nne mwaka 2016 ikilinganisha  na ufaulu  wa  asilimia 67.91 mwaka 2015 na  kuhusu ubora  alisema  daraja kwanza  hadi la tatu waliofaulu  ni asilimia 27.6 tu .


Kwa  upande wake mgeni  rasmi  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza katika  hotuba yake  iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Mufindi  Jamhuri Wiliam  aliwataka  wazazi na walezi mkoani Iringa kuwaandikisha  shule  watoto  wote  wenye umri wa kwenda  shule  pamoja na kutoa  ushirikiano walimu  ili  kuongeza ufaulu  zaidi kwa wanafunzi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE