May 31, 2017

MFUNGWA ALIYEHUKUMIWA MIAKA 63 KWA KUBAKA MZUNGU IRINGA APIGWA RISASI NA POLISI ...................

kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa Julius Mjengi  akifafanua  jambo  wakati  akitoa taarifa ya mfungwa  aliyepigwa  risasi  wakati  akitoroka mahakamani baada ya kufungwa miaka 63  kwa  makosa matatu  likiwemo kumpaka binti  raia wa  kijerumani ,kumfanyia  unyang'anyi  wa  kutumia  silaha na kumpora  simu aina ya Iphone 4
..........................................................................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog 

MFUNGWA  aliyehukumiwa  miaka 63  jela  kwa  kosa la kumbaka  binti  mmoja  raia  wa  Kijerumani Gangilonga  mjini Iringa Rashid  Salufu (23) ajeruhiwa  kwa kuigwa    risasi  za  miguuni na makalioni wakati  akijaribu  kuwakimbia  polisi  kukwepa  kutumikia kifungo hicho   jela.

Imeelezwa  kuwa mfungwa  huyo  mara  baada ya  kusomewa  hukumu  yake na   katika mahakama  ya  hakimu mkazi  mfawidhi  mkoa  wa Iringa alipinga  adhabu   hiyo  mbele ya  hakimu  kuwa hataweza  kutumikia kifungu hicho kwa madai  ni miaka  mingi  sana.


Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa  Julius Mjengi  alimweleza  mwandishi wa matukiodaimaBlog leo  ofisini  kwake  kuwa tukio hilo  lilitokea  Mei 30 majira ya saa 5  asubuhi  mwaka huu  katika viwanja  vya  makakama ya mkoa  wa Iringa  jengo la mahakama  kuu  eneo la Gangilonga  mjini Iringa .

Alisema  kuwa  mfungwa  huyo Salufi  ambae ni mkazi wa Frelimo  katika Manispaa ya  Iringa  alikuwa na kesi CC namba 20/2017  ya  kumbaka  binti   huyo wa  kijerumani (jina  limehifadhiwa) mkazi wa Gangilonga Januari 19 mwaka huu wakati binti  huyo  akielekea nyumbani kwake Gangilonga na baada ya  ubakaji  huyo  alimnyang'anya simu  yake  na  kumtishia  maisha  kisha  kumpora  simu  yake aina ya Iphone 4

Hivyo  alisema kijana  huyo  alikamatwa akiwa na simu  hiyo na  kukiri  kosa  la  kubaka na unyang'anyi wa kutumia  silaha na  kumjeruhi binti  huyo  hivyo kufikishwa mahakamani kwa makosa matatu  hivyo  mahakama  hiyo  ilimfunga miaka 30  kwa  kosa la ubakaji ,miaka  30  kosa la unyang'anyi wa  kutumia sialaha na kosa la  miaka 3  la  uporaji wa  simu  hivyo kulazimika  kutumikia miaka 63 kwa  pamoja .


" Huyu  mshitakiwa  baada ya kusomewa  hukumu  alimweleza  hakimu  kuwa hawezi  kabisa kutumikia  miaka  hiyo 63  aliyohukumiwa ......wakati akitolewa  katika  chumba cha mahakama  kupelekwa mahabusu ya muda mahakamani hapo kabla ya kwenda  kuanza  kutumikia adhabu yake  alijaribu  kutoroka kwa  kujichanganya na  wananchi  waliofika mahakamani hapo na  kutaka  kukimbia  kabla ya  polisi  kufyatua  risasi  hewani  kwa  ajili ya  kumtaka  ajisalimishe  mwenyewe ila  hakuweza  kufanya  hivyo na kutaka  kuendelea kukimbia "


Alisema kamanda Mjengi kuwa kutokana na mfungwa huyo  kuendelea  kukimbia ndipo  askari mmoja aliweza  kuifanya kazi  hiyo kwa umakini na  kufanikiwa  kumpiga  risasi katika makalio  na  mguuni na  kufanikiwa  kumkamata  na  kumpeleka Hospitali  ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa matibabu .

" Ninampongeza  sana  askari  aliyeanikisha  kumkamata  mfungwa  huyo  kwani  bila  umakini wa askari  huyo polisi  tungelaumiwa kuwa  tumemtorosha mfungwa   huyo  aliyefungwa miaka 63  kwa  ubakaji Raia wa  kigeni  waliofika mahakamani hapo  walikuwa  wengi  sana  kufuatilia mwenendo  wa  kesi  hiyo "


Mganga  wa mifupa  katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Charles Lema  alisema  kuwa hali ya  majeruhi  huyo inaendelea  vizuri na  kuwa atakuwepo  wodini kwa wiki  zisizopungua  6  akipatiwa matibabu ya majeraha   hayo kwani  alisema alijeruhiwa paja la kushoto na mkoano wa  kulia .

Alisema hali ya mkono ni nzuri kwani hakuna mfupa  ulioguswa na risasi  hiyo ila mguu wake wa kushoto kuna mfupa ulipata  majeraha  na risasi  moja  ilimpata  jirani na maeneo yake ya  siri .

MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE