May 25, 2017

MCHORAJI WA NEMBO YA TAIFA AANZA KUFANYIWA UCHUNGUZI


unnamed
Mchoraji  Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea Hospitali ya Amana.
A
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara  hiyo  Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dar es salaam                                                     25-05-2017
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji  wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu .
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema  Mzee Kanyasu amechukuliwa leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu ya awali.
‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali yake kiafya sio nzuri hivyo  Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili ‘’ Amesema Dk. Juma.
‘’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi  tutamuanzishia tiba haraka  kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa MNH.’’ Amesema Dk. Juma.
Kwa mujibu wa Dk. Juma  kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa  mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE