May 15, 2017

NI IMANI YA WANANCHI IRINGA MAKANDARASI MLIOLIPWA PESA HIZI BILIONI 1.3 ZA BARABARA MANISPAA YA IRINGA WATAFANYA KAZI NZURI


Manispaa ya  Iringa  imeanza  kutengeneza barabara ya Mtwivila  sekondari  japo  changamoto  kubwa ya barabara   hiyo ni mifereji ya maji  ya  mvua  ndio  huwa inachangia  ubovu wa  barabara hii
Meya wa Manispaa ya Iringa Alex kimbe akizungumza na wanahabari kabla ya kuwasainisha mikataba wakandarasi waliopewa kazi ya kutengeneza barabara mbali mbali za Manispaa ya Iringa 
Baadhi ya makandarasi  waliopewa kazi ya  utengeneza  barabara na  mifereji Manispaa ya  Iringa

ZAIDI  ya  mwezi mmoja sasa Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa mkoani Iringa imewasainisha mikataba wakandarasi 14 kwa ajili ya matengenezo ya barabara mbali mbali za mji wa Iringa .

Mji  wa  Iringa ni  moja kati ya  miji  ambayo inazungukwa na  milima mingi  hivyo ni  wazi barabara  zake  zinahitaji  ukarabati  wa  mara  kwa mara na  ukarabati unaozingatia ubora na Jografia ya mji .

Kutokana na  Mvua  kubwa  zilizopata  kunyesha  kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu  zimepelekea  barabara  nyingi  za mji  wa Iringa  kuharibika na  baadhi  kutopitika  kutokana na ubovu  uliopitiliza hali inayosababisha kero  kubwa  kwa  watumiaji  wa  miundo mbinu ya  barabara  hizo.


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe katika  zoezi la kuwasainisha mikataba hiyo alisema kiasi cha  Shilingi bilioni 1,389,455,041.20 kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo .

Kuwa halmashauri yake imeendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia fedha za mfuko wa barabara. 

"Kazi zinazokusudiwa kufanyika ni matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance works) ikihusisha ujenzi wa barabara ya lami ya Frelimo -Muungano (Routine maintenance works) na ujenzi / ukarabati wa madaraja "

Anasema   kuwa mchakato wa kuwapata wakandarasi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ukifanyika kwa mujibu wa sheria ya manunizi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake na kuwa zabuni za ushindani kitaifa zilitangazwa katika magazeti na website za zabuni ya mamlaka ya uthibiti wa manunuzi ya umma hivyo alitaka wakandarasi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. 

Hivyo Kimbe anawataka  wakandarasi hao kuanza utengenezaji wa barabara hizo na kuwa Manispaa haitasita kusitisha au kuvunja mkataba kwa mkandarasi atakaye fanya kazi chini ya kiwango. 

Kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ya barabara kutarahizisha usafiri wa uhakika katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa ambayo wananchi wake walikuwa wakisumbuka na adha ya usafiri kutokana na ubovu wa miundo mbinu. 

"kwa barabara kuboreshwa tutaboresha usafi wa mazingira, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Iringa pia kurahisisha utoaji na usimamizi wa huduma za jamii kama elimu na afya "

Alisema kazi zitakazofanywa ni utengenezaji wa barabara ya kiwango cha lami Barabara ya Frelimo,na Muungano pia matengenezo ya kawaida ya barabara za kata za Mtwivila, Nduli, Mlandege, Mshindo, makorongoni, Kitanzini Isakalilo, Mvinjeni, Gangilonga, Ilala, Kitwilu, Ruaha, mkwawa, Mkimbizi, Kihesa na maeneo mengine ya mji wa Iringa. 
Orodha   hii juu ni makandarasi   waliokidhi vigezo vya tenda  ya  ukandarasi mjini Iringa na hakuna shaka  kuwa upataji  wao tenda  hizi maana  walioomba ni  wengi ambao  wana sifa kama  zao ila kutokana na nafasi zilizopo  ninyi  mmeaminiwa na  kupewa kazi  hii .

Hivyo kwa  kuwa mmeomba wenyewe kazi hii  ni vema mkajiongoza  wenyewe  kulinda  heshima ya makampuni  yenu kwa  kufanya  kazi  zenye  ubora na  sio mradi kazi maana  iwapo mtafanya  vibaya leo kwa hii kazi ndogo  sina hakika kama mtaaminiwa kwa kazi kubwa hapo mbeleni maana ili makampuni  yenu yaweze kudumu yanahitaji kuendelea kupewa kazi .

Tayari kumekuwepo na maneno mitaani  kuwa  baadhi ya makandarasi wamepigiwa  simu  kuombwa  chochote  kabla ya  kupewa kazi japo hakuna mwenye ushahidi  wa  moja kwa moja yawezekana ni tuhuma tu zisizo na ukweli  ama  ni  tuhuma   zenye  ukweli  uhakika wa  hili  utapatikana katika  utendaji kazi hii mliopewa .

Maana  kazi ambayo  pesa  yake  ina mtu kati ndani yake bila  shaka itafanyika kwa  kiwango  kisicho cha kawaida  maana yawezekana sehemu ya mtaji imetumika  kuhonga ila kazi ambazo haina mtu kati  itafanyika kwa  kuzingatia BOQ maana  kila mmoja atasimamia misingi ya kazi yake .

Tayari   kufuatia maneneo hayo mwenyekiti wa chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema)  Iringa mjini Frank Nyalusi ambae ni  diwani wa kata ya Mvinjeni  alinukuliwa na mwandishi wa makala haya akisema  kuwa iwapo itathibitika kuwa  kuna diwani ndani ya  chama  chake amehusika  kuomba  chochote ili  kumwezesha  mkandarasi kupata  kazi ya barabara  atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuvuliwa uanachama .

Kwa hili  nimpongeze  sana mwenyekiti Nyalusi maana  yupo kwa  ajili ya  kuona  wananchi  wanahudumiwa bora  ila namshauri kujaribu  kufanya uchunguzi wa  kina kuna haya maneno yametoka  wapi na  kujua  ukweli  wake .

Mtandao  wa matukio daima baada ya  kuona barabara  zinaanza  kuchongwa  umepata  kuzunguka barabara mbali mbali kama ya Mapinduzi  kata ya Gngilonga na ile ya kata ya  Mtwivila na Mkimbizi kiukweli  zilikuwa mbaya  sana  kutokana na mvua kuharibu ila sasa  greda  limepita na kufukia mashimo haya  ila si kwa kiwango cha  juu  japo yamefukiwa .

Hivyo nilisukumwa kumtafuta  mstahiki  meya  wa Manispaa ya  Iringa Mh  Kimbe  na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Dr Wiliam Mafwele ili  kuweza  kujibu malalamiko ya  wananchi juu ya ujenzi unaoendelea katika kata  hiyo kwa  greda kupita kusembea  barabara  ovyo  ovyo .

Maswali ya  wananchi yalinifanya kurejea katika mkataba  uliosainiwa mbele  ya macho yangu na mkandarasi Miyomboni  Central Hadrdware Store wa Tsh  milioni 96,686,285 ambao  unaonyesha  kuwa atafanya kazi yaMatengenezo  ya  muda maalum barabara  Mtwivila  sekondari na Mwaikasu ndani ya  muda wa  miezi minne .

Katika  hili  nimejikuta napata  maswali magumu  kuliko majibu kwani majibu ya viongozi  wa Manispaa akiwemo meya na mkurugenzi ni kwamba matengenezo ya  barabara  hiyo mkandarasi kazi  yake ni mifereji wakati Manispaa imejitolea  kusembua barabara  hiyo .

Kimsingi  hakuna  shida  ya Manispaa kujitolea  kusembea  barabara  hiyo ila ni vema katika mkataba  huu na mingine ikawekwa  wazi kwa  kutaja kazi husika  inayofanywa na mkandarasi  kama ni matengenezo ya  mifereji ,au  kifusi ama  kufyeka nyasi ni  vizuri  ikaandikwa  hivyo kuliko kusema matengenezo maalum ya  barabara   wananchi  wakawa na matumaini makubwa ya  barabara  zao  kutengenezwa  kumbe ni  kusembuliwa .

Ushauri  mwingine kwa  wataalam  wetu Manispaa  ilikuwa ni vema  kutengeneza  barabara zikapitika  vizuri na kutengeneza  mifereji sehemu  korofi maana  hali ya barabara  si nzuri  kama mnavyofikiri ninyi kutengeneza mifereji bila ubora  wa  barabara kwa maoni yao ni sawa na kunawa mikono na tope kabla ya  kula .

Kuna  haja ya  kubainisha kazi za makandarasi  hawa  ili  wananchi  waweze  kusaidia kusimamia pale mkandarasi anavyofanya yake  basi  iwe rahisi kutoa  taarifa  pia barabara  hii ya Mtwivila  tumeona  kuna wakandarasi wawili akiwemo Miomboni na Justa ambae  amepsainishwa mkataba wa Tsh milini 71 .7 kwa  ajili ya Matengenezo ya barabara  za Kihesa ,Mkimbizi na Mtwivila .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE