May 24, 2017

DC KILOLO AMPIGA STOP MWEKEZAJI ALIYEUZIWA MLIMA , MWENYEKITI ANUSURIKA KUTUPWA MAHABUSU ....

Mkuu wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  akiwahutubia  wananchi wa kata ya Ilula  leo
Diwani  wa kata ya Ilula Reymond Francis kushoto  akifafanua  jambo  mbele ya Dc  Kilolo Asia Abdalah  anayeandika 
Wananchi wa kata  ya Ilula  wakiwa katika mkutano wa DC Kilolo
Mwenyekiti wa kitongoji cha Madizini Ilula Paul Mpichi   kulia  akiwa  chini ya ulinzi wa  polisi baada ya  kutuhumiwa kuuza hifadhi ya mlima na wakati wa mkutano wa DC hakuweza  kutokea kabla ya  kutafutwa na polisi na kuletwa mkutanoni hapo kwa amri ya  polisi  ili  kujibu  tuhuma zake  za kuuza mlima  kwa  kutumia majina ya  viongozi wa wilaya na mkoa
Wananchi  wakisikiliza kwa makini mkutano wa DC  Kilolo
Dc  Kilolo  Asia Abdalah  akiwahutubia  wananchi wa Ilula
Wananchi wakitoa malalamiko  yao kwa Dc
Mkazi wa Ilula  akilalamika kwa mkuu wa wilaya ya  Kilolo baada ya motto  wake  kufukuzwa shule kwa  kukosa pesa ya mchango wa uji
Na MatukiodaimaBlog
MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani  Iringa  Asia Abdalah apiga marufuku  mwekezaji  aliyeuziwa  hifadhi ya mlima wa  Madizini Sabato kata ya  Ilula  wilayani  Kilolo  kuendelea na kilimo katika  mlima   huo na badala yake kutakiwa kuondoka  mara moja  katika   hifadhi   hiyo  ya  mlima


Huku  akiagiza ungozi wa  kata ya Ilula  kusimamia kufutwa kwa  kesi  zote  zilizofunguliwa mahakamani na aliyekuwa afisa  mtendaji wa  kitongoji  cha Madizini kwa wananchi  waliokuwa  wakipinga mlima  huo kuuzwa kwa  mwekezaji.

Akitoa  maagizo hayo leo  kufuatia  malalamiko ya wananchi juu ya  viongozi  wao  wa kijiji  kuuza hifadhi  hiyo ya  mlima huo    wakati wa mkutano wa hadhara  uliofanyika mjini Ilula mkuu  huyo  wa wilaya   kabla ya  kutoa agizo hilo  aliagiza  jeshi la polisi kwenda kumkamata mwenyekiti  wa  kitongoji cha Madizini Paul Mpichi  aliyetuhumiwa kushiriki  kuuza mlima  huo kwa  kutumia majina ya  mkuu  wa wilaya,mkuu  wa mkoa na kamanda  wa polisi   kuletwa mkutanoni  hapo .

Mkuu  huyo  alisema amesikitishwa na hatua ya viongozi wa  serikali ya  kitongoji cha Madizini  kutumia majina ya  viongozi  wa wilaya   hiyo  na mkoa  katika  uuzaji wa  hifadhi hiyo yam lima jambo  ambalo ni uzushi na utapeli  wa hali ya  juu .

Alisema kutokana na maelezo ya  wananchi  yaliyotolewa mbele  yake mkutanoni hapo  mwenyekiti   huyo baada ya  kubanwa  kwenye mkutano  wake  na  wananchi alidai kuwa baraka  za  kuuza mlima  huo  zaidi ya hekari 20 alizipata kutoka ofisi ya mkuu wa  wilaya ya Kilolo, mkuu wa mkoa wa Iringa na kamanda  wa  polisi  wa mkoa huku akijua ni uongo na alifanya  hivyo kutisha  wananchi ili  wasiendelee kuhoji  zaidi.

“  Mimi nimekuja  hapa  wilaya  ya  Kilolo  kwa  kuaminiwa na mheshimiwa Rais Dkt  John Magufuli pia  mkuu  wangu wa mkoa Amina Masenza nataka  unieleze  ni  lini  umekuja ofisini  kwangu na umekwenda  ofisi ya  mkuu  wangu wa mkoa na kamanda  wa polisi  tukakuruhusu  wewe  kuuza mlima “  

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE