May 28, 2017

MASHINDANO YA RITTA KABATI CHALLENGE CUP ,SERIKALI TUTAYAUNGA MKONO - RC IRINGA

Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza (kulia)  akipiga mpira  kufungua mashindano ya  Ritta Kabati  Challenge Cup 2017  leo katika uwanja wa Kreluu  mjini Iringa golini ni mbunge  Kabati ambaye  mdhamini  wa mashindano hayo na katikati ni mkuu wa wilaya ya Iringa  Richard Kasesela ambae  alikuwa ni muamuzi wa ufunguzi huo 
Mkuu wa  wolaya ya Iringa Richard kasesela  kulia  akisalimiana na madiwani wa Chadema waliofika katika uzinduzi wa mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup  leo kulia kwake ni mbunge wa  kilolo Venance Mwamoto , Baraka  Kimata  na  Leah 
Mwenyekiti wa Chadema Iringa mjini Frank Nyalusi  kulia akiwa na viongozi mbali mbali meza kuu
<
Mwanahabari wa radio  Ebony Fm Stella Ngenji aliyefika  kufuatilia mashindano hayo 
Dereva  wa DC Iringa Bw  Rama akifuatilia mashindano hayo akiwa katika gari 

Mwenyekiti wa  kamati ya mashindano Gerald Malekela  akisoma  taarifa ya mashindano  hayo 
Kamati ya  mashindano hii hapa 

Mwenyekiti wa IRFA  Cyprian Kuyava akipongeza mashindano hayo 
Mwakilishi wa meneja wa NSSF  mkoa wa Iringa 
Mbunge Rita Kabati akieleza  sababu ya  kuanzisha mashindano hayo 
Kamanda wa  polisi mkoa Julius Mjengi wa tatu  kulia akiwa na mbunge wa kilolo Mwamoto kushoto na viongozi  wengine 
Mbunge Kabati  akifafanua  jambo 
Rc  Iringa Amina Masenza akifungua mashindano hayo 
Hawa ni  viongozi wa  timu shiriki  
Rc  Iringa  akigawa  vifaa vya michezo kwa viomgozi wa  timu  zinazoshiriki mashindano hayo 
Mwenyeki  wa chama cha waamuzi mkoa wa Iringa Ramadhan Mahano  akikaribisha viongozi kuzindua mashindano hayo 
RC  Iringa Amina Masenza  akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kibwabwa FC 
Diwani Kimata  akiwa na timu yake wakati mbunge Kabati akisalimiana na wachezaji 
Mgeni Rasmi  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisalimina na wachezaji wa timu ya Kihesa Fc ambayo imeshinda mchezo huo kwa goli 1-0
RPC Iringa Julius Mjengi  akisalimiana na  timu ya Nduli FC 
Mkuu wa  mkoa na  viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa KIhesa FC 
Rc  Iringa akimpongeza mwamuzi wa kitaifa kutoka mjini Iringa Janeth Balama  ambapo mkoa unakusudia kumwezesha kupitia wadau ili awe mwamuzi wa kimataifa 
Mbunge Kabati  akimpongeza Muamuzi Janeth 
RC akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Kibwabwa FC 
Dc Kasesela  akijiandaa kupiga mpira  
Mbunge Venanve Mwamoto na Ritta Kabati  wakiwa  golini kujiandaa kudaka 
Mlinda mlango Kabati  akijaribu kudaka  mpira  uliopigwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza 

RC Iringa akipiga mpiga  kufungua mashindano ya Kabati Cup 
Janeth Balama  akiwajibika 
Makamu  mwenyekiti wa Bavicha Taifa  Patrick Ole  Sosopi katikati akimpongeza mbunge Ritta Kabati kwa kuanzisha mashindano hayo  kulia ni mwenyekiti wa chadema Iringa mjini Frank Nyalusi 

Na  MatukiodaimaBlog
SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa imeagiza  wakuu  wa  wilaya  kutoa  ushirikiano kwa waandaaji  wa mashindano  makubwa  ya  kisoka  mkoani Iringa  ya   mbunge  Ritta Kabati chalenge  Cup  2017 ambayo  yameanza  kutimua  vumbi leo  mjini Iringa kwa  kuzishirikisha  timu  46  kutoka mkoa huo.

Akito  agizo hilo  leo  kwa  niaba ya  waziri wa habari ,utamaduni ,sanaa na michezo Dkt  Herrison Mwakyembe  aliyepaswa  kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo katika  uwanja wa chuo  cha ualimu Kreluu  mjini hapa ,mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  alisema  kuwa  kuanzishwa kwa mashindano hayo ni  fursa  kubwa kwa  vijana  kuonyesha uwezo  wao katika michezo na mwanzo wa ajira .

Hivyo  alisema kuwa lazima  serikali za  wilaya  zote za  mkoa huo kutoa  ushirikiano kwa  waandaaji  wa mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kuziwezesha  timu  zinazoshiriki  kufika kwenye  viwanja  vya mashindano na wilaya ya  Mufindi   kuhakikisha  timu ya JKT  Mafinga  kushiriki mashindano  hayo .

Hivyo  alisema atamuagiza  mkuu wa wilaya ya  Mufindi  Jamhuri  Wiliam kuhakikisha  timu  ya JKT  inashiriki mashindano hayo na kuungana na  timu 46  zinazoshiriki  ikiwemo timu ya Polisi  na  ile  ya  kikosi cha zimamoto na uokoaji  ambazo  zimeshiriki katika  mashindano hayo.

Aidha  mkuu  huyo  wa  mkoa alionya  timu  zinazoshiriki mashindano hayo  kutumia  michezo  hiyo  kuonyesha  uwezo  wao katika  soka na  sio  kutumia michezo  hiyo  kufanya  vurugu na kuwa timu  ambayo  wachezaji  wake  watafanya  vurugu  watachukuliwa hatua kali  za  kisheria kwani  hatapenda  kuona michezo  hiyo   inakuwa  sehemu ya  vurugu .

Alitaka  waratibu wa  michezo hiyo  kutoaonyesha  upendeleo ama  kuwa sehemu ya kuvuruga michezo  hiyo ambayo iwapo itafanyika  salama kwa kila timu  kuonyesha  uwezo  wake ni moja ya  fursa  kubwa kwa  mkoa wa Iringa katika michezo .

Pia  mkuu  huyo wa mkoa aliahidi  kuwasaidia waratibu hao pamoja na  kuangalia  uwezekano wa  serikali ya  mkoa  wake  kuunga mkono  zaidi  michezo  hiyo.

Akizungumza  uwanjani hapo  mdhamini wa mashindano hayo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema  kuwa uanzishwaji  wa mashindano hayo ni  mawazo ya  wanahabari wa  michezo  mkoa wa Iringa ambao  ndio  walikuja na wazo la kuwa na mashindano hayo na  yeye  kuamua kuunga mkono kwa  kujitolea  kufadhili mashindano hayo pamoja na wadau  mbali mbali  ikiwemo kampuni ya  pikipiki ya  SuN LG  ambao  wamejitolea  zawadi kwa mshindi  wa  kwanza na  wengine  ambao wameahidi  kujitokeza kudhamini mashindano  hayo .

Alisema kuwa  kuanzishwa  kwa mashindano hayo ni  fursa  kubwa kwa  vijana  wote  bila kutazama  vyama vyao  kushiriki  kutangaza  vipaji vyao  ili  timu mbali mbali  kupata  wachezaji kupitia mashindano hayo ambayo  wamewashirikisha  viongozi  mbali mbali wa  timu   kubwa za  mkoa wa Iringa  kufika  kusajili  wachezaji .

Pia  alisema moja kati  ya  taratibu ya mashindano hayo ni  kuwapatia  elimu  mbali mbali ikiwemo ya ujasilia mali na  dawa  za  kulevya kama  njia ya  kuwaepusha na matumizi ya dawa za kulevya  pia  kupanua  uwezo wa kuanzisha  shughuli  za  kiuchumi .

Mbunge Kabati  alisema mashindano  hayo yatakuwa  endelevu na  baada ya kumalizika kwa mashindano hayo timu  hizo hazitavunjwa na badala yake  kupitia  elimu  watakayoendelea  kupewa  shauku  yake  kuona  vijana hao  wanakuwa na vikundi  vya  kiuchumi .

Mwenyekiti wa Chama Cha soka Mkoa wa Iringa (IRFA) Cyprian Kuyava alipongeza  ujio wa mashindano hayo na  kuwa mashindano hayo ni makubwa sana na yanashirikisha  timu  nyingi kuliko hata  ligi  kuu ya VPL iliyomalizika ambayo  ilishirikisha timu 16  pekee  hivyo  alisema wao kama chama cha  soka  mkoa  wamepokea kwa  mikono  miwili mashindano hayo na  watayaunga  mkono kwa  kuongeza zawadi kwa  washindi .


Mashindano hayo  ambayo  yameonyesha  umoja na mshikamano kwa  vyama vya siasa mkoa wa Iringa baada ya  chama cha Demokrasia na maendeleo  (Chadema) wilaya ya  Iringa mjini kupitia mwenyekiti wake Frank Nyalusi  pamoja na baadhi ya madiwani wa chadema  mjini hapa  kushiriki kwa mara ya kwanza  shughuli zinazoandaliwa na mbunge wa CCM tofauti na awali  ambapo kila chama  kilikuwa  kikijitenga .


Mbali ya  wapinzani  kuonyesha  ushiriki  wao katika  tukio hilo bado diwani wa Chadema kata ya  Kitwiru Baraka Kimata ambae ni katibu mwenezi wa Chama  hiyo mkoa   alionekana kuunga mkono  kwa  kuleta  timu yake uwanjani ,pamoja na kimata pia makamu mwenyekiti wa baraza la vijana  wa Chadema Taifa Patrick Ole  Sosopi alipata  kushiriki kushuhudia uzinduzi  huo.

Akisoma taarifa ya mashindano hayo kwa niaba ya kamati  ya mashindano  Gerald Malekela  alisema kuwa mashindano hayo  yamewaunganisha  pamoja   yana  wachezaji  1150  na  viongozi 50 hivyo  kufanya  jumla ya  fursa  kwa  vijana 1200 kushiriki mashindano hayo .

Alisema  timu 23 zinashiriki  kutoka Manispaa ya Iringa ,tumu 9 kutoka Iringa  vijijini ,timu 13 kutoka  wilaya ya  Mufindi na  timu moja  kutoka  wilaya ya  Kilolo .

Kuhusu  zawadi kwa  washindi alisema mshindi wa kwanza atapewa  pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 2na jezi seti  moja  ,mshindi wa pili atapewa pesa  shilingi 500,000na seti ya  jezi na mshindi wa tatu atazawadiwa  kiasi cha shilingi 250,000 na seti ya  jezi .


Pia  mshangiliaji  bora ataondoka la  shilingi 100,000,mchezaji bora na mfungaji  bora  shilingi 50,000 huku timu zitakazo ingia nane bora kila mmoja itapewa  seti ya jezi na  kutakuwa na zawadi kwa muamuzi bora .

Katika  mchezo  huo wa ufunguzi  timu ya Kibwabwa FC imejikuta  ikigagaduliwa kwa  jumla ya  goli 1-0 na  timu ya Kihesa  Fc ambayo  imeanza mashindano hayo kwa  kicheko na kujinyakulia  zawadi ya  shilingi 50,000 kutoka kwa mwenyekiti wa timu ya wabunge wa  bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Venance  Mwamoto ambae ni mbunge wa jimbo la Kilolo .

MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE