May 21, 2017

TIMU ZAIDI YA 40 KUSHIRIKI LIGI YA RITTA KABATI CHALLENGE CUP 2017


Baadhi  ya  viongozi  wa  timu  zitakazoshiriki  ligi ya Ritta Kabati Chalenge Cup  wakiwa katika  semina elekezi
Waratibu wa mashindano  hayo wakitoa kanuni za mashindano

 Na MatukiodaimaBlog
JUMLA    timu zaidi 40  mkoani  Iringa  zinataraji  kushiriki mashindano ya mbunge Ritta Kabati Callenge  Cup 2017 yanayotaraji  kuanza  kutimua  vumbi katika  viwanja  mbali mbali  vya  mkoa wa Iringa.

Mratibu  wa mashindano hayo Fredy  Mgunda  akitoa kanuni  za mashindano  hayo alisema   kuwa katika mashindano hayo yenye  lengo la kuibua  viwango vya  michezo ndani ya mkoa wa Iringa na  kuwaepusha  vijana na matumizi ya  dawa  za  kulevya mshindi  atazawadiwa zawadi ya  boda  boda  mpya  na mshindi wa  pili atapewa mashine ya kufyatua  tofari  wakati mshindi wa tatu ataondoka na kombe .

Alisema  kuwa mashindano  hayo  yataendeshwa  kwa  kufuata sheria zote za  kumi na  saba  za mpira  wa miguu na  yataendeshwa kwa mfumo  wa  ligi kabla  ya  kuanza  kwa mtoano na  kuwa  timu  zote  zitakazo shiriki  mashindano hayo  zitatakiwa  kuzingatia taratibu  zitakazo  wekwa na kamati ya mashindano  hayo .

" Kamati ya  mashindano hayo  ndicho  chombo cha juu cha rufaa dhidi  ya malalamiko  yote katika mashindano hayo ....ada  ya  rufaa itakuwa ni shilingi 50,000 ambayo lazima zilipwe ndani ya masaa 24 baada  ya  kumalizika kwa  mchezo  husika"

Aidha  alisema  waamuzi watakaovuruga mchezo  wataondolewa kuendelea  kuchezesha michezo hiyo hiyo pia timu itakayo fanya  vurugu  kupelekea  mchezo  kuvunjika ama kuvunjwa itaondolewa  kwenye  mashindano  hayo.

Pia  alisema   kuwa  timu  zinazotarajiwa kushiriki katika mashindano  hayo ni kutoka katika wilaya  zote za mkoa wa Iringa na  kuwa kuanzishwa kwa mashindano hayo  kutatoa fursa kwa  vijana wengi  kushiriki katika mashindano hayo  na kutumia mashindano hayo kama  sehemu ya  kuonyesha  vipaji  vyao ili  kujipatia ajira kupitia  soka.

Mgunda  alisema  kuwa  miongoni  mwa timu  zinazoshiriki mashindano hayo ni  pamoja  na  timu ya  Zimamoto katika manispaa ya  Iringa na timu nyingi  mbali mbali za wilaya ya Iringa ,Kilolo na Manispaa ya  Iringa .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE