May 28, 2017

MAREKANI KUFANYA MAJARIBIO YA KUNDUNGUA KOMBORA


                             

Mfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini
                                     Mfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini
Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine.

Maafisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki ijayo.


Kumekuwa na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.


Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.
Matamshi hayo yanaonyesha wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wa Pyongyang wa kutengeza makombora mbali na mpango wake wa Kinyuklia, ambayo Korea Kaskazini inasema inahitaji kwa ulinzi wake.


Maafisa wa Marekani wanasema kuwa majaribio hayo yalipangwa mapema na kwamba haijibu kisa chochote.


Pentagon ilitangaza jaribio hilo wakati ambapo Korea kaskazini inatengeza kombora la masafa marefu.
                                     Makombora ya Korea Kaskazini
Ni mara ya kwanza Marekani kujaribu kuzuia kudungua kombora la masafa marefu ICBM.
Marekani imekuwa ikitumia kifaa cha GMD kinachowekwa ardhini kukabiliana na mashambulio ya mataifa kama vile Korea Kaskazini.


Lina uwezo wa kudungua makombora mengine lakini hawajajaribu kudungua makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.


Huku maafisa wa Marekani wakiamini kwamba Pyongyang ina miaka mingi ya kuweza kufanikiwa kutengeza kombora la masafa, marefu ICBM , wanaamini taifa hilo limepiga hatua.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE