May 13, 2017

MAPACHA WALIOUNGANA WAHITAJI MUME WA KUZANA NAO WATOTO WATATU ....

Mapacha  walioungana  Maria na Consolata   wakizungumza  kwa  njia ya simu na mmoja kati ya  wasamaria  aliyewachangia kiasi cha  pesa  kupitia  simu  yao  ya kiganjani
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abadalah kushoto  akizungumza na mapacha  hao
Mlezi  wa mapacha  Maria a Consolata  akiwatoa  darasani kushoto ni mkuu  wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah picha  zote na matukiodaimaBlog
 
Na MatukiodaimaBlog
 
MAPACHA Maria  na  Consolata Mwakikuti (26)walioungana  kiwili  wili na  kuwa na  kila mmoja  kichwa  chake ,mikono yake na miguu  miwili  waliohitimu  kidato cha  sita  shule ya sekondari  Udzungwa wilaya ya  Kilolo  mkoa  wa Iringa jana  wamesema  wanatamani kuwa kuja kuwa  walimu ili  kulipa fadhila kwa  jamii kwa kuwafundisha  watoto wao

Huku  wakisema hitaji  lao  ni kuwa na watoto  watatu  pekee  hivyo pindi  watakapomaliza  chuo  kikuu  wakianza  kujitegemea  watahitahi mwamaume wa kuwaoa ili kuanza  safari ya  kutafuta  watoto hao  watatu .
Mapacha  hao  walisema  hayo jana  baada ya   sherehe ya  kuwaaga  iliyoandaliwa na mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani  Iringa  Asia Abdalah kama  sehemu ya  kuwatia moyo   mapacha  hao shuleni hapo.

Wakizungumza mara baada ya  sherehe hiyo   fupi  Maria  na Consolata  walisema wanampongeza  mkuu  huyo wa  wilaya  kwa  kuonyesha  kuwajali na  kuwa   wanataraji  kuendelea na masomo ya  chuo  kikuu na  baada ya  kumaliza  masomo ya chuo  kikuu  wanategemea   kuifanya kazi ya  ualimu  na baada ya hapo kuuendesha maisha yao  wenyewe kwa  kuolewa na kuwa na watoto  watatu  pekee .

Mapacha  hao  walimuomba mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  kuwakutanisha  na makamu  wa rais  wa Jamhuri ya  muungano wa Tanzania Samia Suluhu  Hassan ama  Rais Dkt  John  Magufuli  ili  kufikisha  ombi lao  la kuomba  kusaidia  kuifanyia  ukarabati  shule ya  sekondari Udzungwa na kusaidia  kutatua  kero   ya  vitabu  vya masomo ya  sayansi shule  za  sekondari nchini .

"Mheshimiwa  mkuu  wa  wilaya tunaomba sana  viongozi  kuendelea  kuwa  waadilifu kama  ilivyo kwa   Rais  wetu Dkt  John Magufuli mzee  wa  hapa kazi Tu .....tunatambua   wewe  mkuu wa wilaya  ni muadilifu sana na ndio maana  uliahidi na  umetimiza ahadi yako ya  kutusaidia  na  kuwaandalia wanafunzi  wenzentu chakula muda  wote  wa mitihani ......ila  tunaomba iwapo makamu  wa rais atafika  Kilolo basi tumsubiri tukutane nae au  tufikishie  salamu  zetu kwa rais na maombi yetu hayo "  walisema  mapacha  hao  huku  wakishuka  chini ya  kochi  walilokuwa  wamekaa na  kupiga magoti .

Walisema  wanashukuru wadau  wote  ambao  wamepata  kuwasaidia  toka  wakianza  elimu ya  sekondari  wilaya ya  Kilolo wakiwemo Hamashauri ya  Kilolo  ambao  walijitolea  kujenga  nyumba  yao  maalum pia  kituo  cha  Nyota  ya asubuhi  na wengine wote  kwa misaada mbali  mbali  waliyoipata wakiwa  shuleni hapo .

Kwani  walisema  wamepata  kuishi vizuri pamoja na kuwa   wao ni  watoto  watatu kati ya  watoto 5  wa  familia ya Mwakikuti ambao  kwa  sasa  walikwisha  fariki  dunia  wote wawili kwa maana ya mama  na baba  waliokuwa  wakifanya kazi ya ubwana shamba na bibi  shamba  wilaya ya  Makete wakitokea  mkoa wa Mbeya.

Walisema  maendeleo yao  mazuri  shuleni hapo ni  kutokana na faraja  kubwa ambayo ilikuwa ikionyeshwa na wasamaria  wema  mbali  mbali na kuwa imani  yao  kubwa na  kupata  matokeo  mazuri  zaidi katika mtihani  huo  wa kidato cha  sita .

Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia  mbali  ya kuwapongeza  kwa kutambua michango mbali mbali ya  wahisani  bado  alisema iwapo  makamu  wa Rais  wakati wa  ziara  yake  wilaya ya  Kilolo atamuomba mkuu  wa  mkoa  wa Iringa ili  kumwomba mkamu  wa  Rais kupita kuwasalimia mapacha hao .
 
Alisema  kuwa pongezi nyingi  walizotoa kwa  serikali ya  awamu ya tano  chini ya Rais Dkt  Magufuli  zitamfikia na  kuwa bado  serikali ya awamu ya  tano  ipo  kwa ajili ya  watanzania wote na  kuwa ili  kumuunga mkono  Rais ,mkuu  huyo  wa  wilaya  alitaka  wahitimu wa  kidato cha sita   shuleni hapo kuhakikisha wanaachana na mpango  wa kukimbilia  kuolewa na badala yake  kuendelea na masomo  zaidi .
 
Mkuu   huyo  wa  wilaya  alitaka wahitimu hao  kuwa mabalozi  wema kwa  Taifa kwa  kujiepusha na matendo  yasiyo faa kama  utumiaji  wa dawa  za  kulevya na mengine yanayofanana na  hayo yasiyo  mema kwa  jamii. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE