May 11, 2017

MAPACHA MARIA NA CONSOLATA WALIOUNGANA KIWILIWILI NA KUTUMIA MIGUU MIWILI ,MIKONO MINNE VICHWA VIWILI WAELEZA MAKUBWA

Mapacha  Maria  na  Consolata  wakiwa katika  nyuso  za  furaha leo  baada ya  kumaliza mitihani ya kidato cha  sita  na  kutembelewa na mkuu wa  wilaya ya kilolo Asia Abdalah
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akiwa na viongozi wa  bank  ya  NNMB Kilolo na kanda wakiwapongeza  mapacha hao
Mapacha  hao  wakiwa  katika  furaha  kubwa leo
Na MatukiodaimaBlog
HUJAFA  hujaumbika na siku zote  Mungu  ni mwema na Mungu ana makusudi yake  ni  wa ajabu kwa sababu maajabu yake ni makubwa na ukuu  wa Mungu unajidhihirisha katika muujiza wa watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana kiwili wili Consolata na Maria Mwakikuti  ambao sasa wana ndoto ya kujiunga chuo kikuu.

Ikumbukwe  kuwa mapacha wengi wanaoungana hudumu kwa kipindi kifupi na wengine hupoteza maisha wakati madaktari wakijaribu kutumia ustadi wao wote kuwatenganisha ila  wapo ambao Mungu huwaruhusu kuendelea na maisha na kuwapa mafanikio  ya tele katika maisha yao .

Hivyo miongoni mwa mapacha walioungana na ambao hadi sasa wanaishi  na kufanya vizuri kwenye masomo yao  Consolata na Maria ambao ni  miongoni  mwa  watoto 6 kwenye familia ya Mwakikuti na  Mungu, si tu, amewaruhusu kuendelea kuishi, bali pia ameanza kuonyesha maajabu yake kwa kuwapa mafanikio na kufanya  vizuri kwenye masomo yao


Mapacha  hawa   wameungana kuanzia  kiunoni  wanatumia  miguu  miwili ,mikono mine  kila mmoja na yake  na  vichwa  viwili  kwa maana  kila mmoja na  kichwa  chake ni  wacheshi  na wanaopendana  kupita  kiasi .


Hawa ni watoto kutoka Ikonda wilayani Makete mkoani Iringa Siku tuliposikia kwamba tumefaulu hatukulala kwa furaha, tuliruka na kumshukuru Mungu kwani hatukuamini kama tungeweza kufaulu kutokana na kusomea katika mazingira magumu sana, anasema Consolata. Hatukua na kiti cha kukalia darasani, siku zote tulikalia kibaiskeli ambacho hakitutoshi na kadri siku zilivyokuwa zikisogea ndivyo kilivyokuwa kikituumiza kwa kuwa ni kidogo,

Kwa mujibu wa mabinti hawa, kila asubuhi rafiki zao waliwapitia ili kuwapa msaada wa kusukuma baiskeli yao hadi shuleni. Muda wa mapumziko waliwarejesha nyumbani kwao kwa ajili ya kujisaidia.
 
Mapacha hao walipata alama zinazolingana kwenye mtihani wao wao mwisho, kila mmoja akipata alama 151, lakini kinachothibitisha kuwa hawakutazamiana wala kusaidiana kwenye mtihani ni kutofautiana kwao kwa alama kwenye baadhi ya masomo.

Katika somo la maarifa ya jamii, Consolata alipata alama 29 na Maria kupata alama 25, wakati kwenye somo la sayansi Maria amemzidi Consolata kwa kupata alama 31 dhidi ya 29 na hali ni kama hiyo kwenye somo la Kiingereza ambalo Maria amepata alama 36 na kumzidi Consolata aliyepata alama 34.

Consolata na Maria ambao kwa  sasa wamehitumu kidacho  cha  sita shule ya  Udzungwa wilayani Kilolo mkoa wa  Iringa   na shauku ndoto  yao  kuendelea na masomo ya  chuo kikuu.

 Mapacha hao walizaliwa mwaka 1996 kijiji cha Ikonda wilaya ya Makete mkoani Njombe walipata elimu yao ya msingi kijijini hapo na kufanikiwa kufaulu vizuri kabla ya mwaka 2011 kuchukuliwa kwa malezi na wamisionari hao na kuletwa wilayani kilolo kwa ajili ya kuwalea zaidi. 
 
Wengi wamekuwa wakitamani  kujua  historia ya hawa   mapacha walioungana kiwiliwili baada ya kimya chao cha muda mrefu wengi watapenda kujua wako wapi na wanafanya nini kwa sasa  mtandao  wa  matukiodaimaBlog umevunja  ukimya  huo na  sasa  kuwa  na undani  wa makala  haya kuwa .
 
Mapacha  hawa  Maria Mwakikuti na Consolata Mwakikuti wamehitimu  kidato cha  sita kwenye shule ya sekondari ya Udzungwa na wanalelewa na kituo cha Nyota ya Asubuhi  Kidabaga, wilayani Kilolo mkoa wa  Iringa.
 
 Mapacha  hao ndoto  yao kubwa  pindi  watakapo maliza chuo  ni kuwa  walimu  tofauti na  awali walipotamani  kuwa ni wataalam wa kompyuta walijiunga na shule ya sekondari Nyota  ya Asubuhi  baada ya walezi wao kukataa wasijiunge na shule ya sekondari ya Jangwani walikokuwa wamepangiwa baada ya matokeo yao kutoka

Mapacha hao wanasema Kuwa wapo yatima wanaoteseka kwa kukosa msaada huku baadhi ya jamii ya Kilolo ikipata tabu ya huduma ya afya hivyo kuomba serikali kuzidi kuboresha huduma za afya vijijini. 

Kuhusu jitihada zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli mapacha hao wanaomba serikali kuendelea kuwatumikia kwa kasi hiyo watanzania japo wanapenda kuona  serikali ikiendelea kuboresha elimu mashuleni kwa kutatua changamoto ya vitabu vya sayansi ili kuzalisha wasomi zaidi wa masomo ya Sayansi nchini.

Wanasema  hawajawahi kufeli somo masomo na wamekuwa wakipishana  iwapo  mmoja atashika upili basi mwingine  hushika ukwanza  darasani na wamekuwa wakishindana hivyo  hadi wanahitimu kidato cha sita.

Wameungana, lakini kila mmoja nahisia zake Juhudi zao zinazolingana katika masomo na tabia zao hazikuwafanya  watu wa aina moja licha ya kuungana tumbo Kila mmoja ana hisia zake na ana vitu anavyopendelea mfano  Maria ni mcheshi zaidi ya Consolata  hachagui chakula lakini Maria akila samaki anasumbuliwa na tumbo.
 
Lakini kama mmoja akijisikia kwenda kulala, basi mwenzake pia atalazimika kulala kwa kuwa wameungana tumboni. Maumbile yao yanawalazimu mapacha hawa  wapendane na kusaidia.

Maria akiumwa, inanibidi niwe mpole, nitulie kwa sababu nikimfanyia fujo nitamuumiza anasema Consolata  kuwa akitaka kulala tunaenda wote na kama litamuuma tumbo la kuharisha basi tutaenda wote uani, hatujawahi kugombana, tunapendana sana.
 
Huku Maria anasema maisha yao ya shule yalikuwa mazuri kutokana na ukweli kwamba, watu wengi waliwapenda hivyo hawakuiona tofauti.

Ifahamike  kuwa ingetegemewa kwamba katika dunia yao la utandawazi na uwingi wa vyombo vya habari, taarifa za kuzaliwa kwao zingepamba magazeti mengi, redio na televisheni.lakini haikuwa hivyo kwa Maria na Consolata ambao walizaliwa Hospitali ya Misheni ya Ikonda mwaka 1996. Ulemavu wao ulisababisha wafichwe na kwa wakati huo habari za kuzaliwa kwao hazikuenea sana.

Walianza kujulikana wakati walipojiunga na elimu ya msingi wakati wamisheni walipolazimika kuwahamishia watoto hao kwa mama mlezi wao na kwa wakati huo, walitafutwa walezi wawili.

Wakiwa na miaka mitatu, baba yao Alfred Mwakikuti alifariki dunia na walipofikia darasa la pili mwaka 2002, mama yao pia alifariki dunia hivyo kuwaacha wakiwa yatima. Mama yao mlezi anasema licha ya kuwa analipwa kiasi kidogo cha mshahara kutoka misheni kwa ajili ya kuwalea, bado maisha yao ni magumu sana na analazimika kulima ili aweze kukidhi mahitaji yao.

Tunahitaji shule ambayo itaweza kutusaidia, kama kuna uwezekano wa kupewa nyumba tutashukuru kwani hali yetu ilivyo ni tofauti na wenzetu. Walimu wao wanashauri, ikiwa Serikali itaamua kuwasomesha, basi ihakikishe kuwa mama yao mlezi anakuwa nao karibu baada ya kuwawezesha kufikia hapo walipo sasa.

Katika maisha yao ya kusoma, kila mmoja alikuwa na madaftari yake na wakati wa kufanya mazoezi au kuandika kazi wanazopewa, mmoja huanza kuandika, akimaliza na mwingine huandika.

“Wala hatupati shida tumezoea, kila mmoja anafanya kazi yake, mimi naandika kwa mkono wa kushoto na Maria anaandika kwa mkono wa kulia,” anasema Consolata, ambaye anaonekana kuwa mchangamfu zaidi.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo  Asia Abdalah , leo  may 11 2017  amepata  kutembelea shuleni  hapo na  kutoa msaada  wa chakula pamoja na viongozi  wa  bank ya  NMB Kilolo   mkuu wa  wilaya anasema kuwa serikali inawathamini na inaendelea kuwapenda hivyo kama mkuu wa wilaya ataendelea kufika kuwasalim na kuwasaidia iwapo  wataendelea  kubaki  chuoni  hapo  kabla ya  kwenda chuo kikuu 

"Nimefurahi sana kuwaona mkiwa na furaha kubwa na mnafanya vema katika msomo yenu kwa kufanya vizuri katika msomo yenu ya kidato cha nne na sasa wapo kidato cha sita "

Alisema kuwa watoto hao mapacha wanaonyesha matumaini makubwa ya kwenda chuo kikuu kutokana na jitihada zao darasani na kuwa wanafanya vizuri masomo yao ya kidato cha sita sasa. 

Itaendelea  Kesho  usikose  ..................................

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE