May 15, 2017

MANISPAA YA IRINGA YATOLEA UFAFANUZI KUHUSU BARABARA YA MTWIVILA SEKONDARI


Mkurugenzi  wa Manispaa ya  Iringa Dkt Wiliam Mafwele  katikati  akimwelekeza jambo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kushoto na mhandisi wa Manispaa  hiyo Mashaka Luhamba
Meya Alex Kimbe
Na  MatukiodaimaBlog
BAADA ya  wananchi   ya baadhi ya  wananchi  wa kata ya Mtwivila katika Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  mkoani Iringa kulalamikia  ukarabati mbovu  wa  barabara ya Mtwivila  sekondari  uliofanyika ,mstahiki meya wa Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe amesema kuwa ukarabati  uliofanyika hauna mahusinano na kiasi cha shilingi  milioni 96.3 alizosaini mkataba mkandarasi .

Akizungumza na  mwandishi wa habari hizi jana , Kimbe alisema  kuwa barabara  ya Mtwivila sekondari na barabara  nyingine  ambazo  ziliharibiwa  na mvua zimesembuliwa na greda la  Manispaa ili  kuwawezesha  wananchi  kuendelea  kupata  huduma ya  usafiri wa  dala dala kama  kawaida .


Kimbe alisema mkandarasi Miyomboni  Central Hadrdware Store ambae amesaini mkataba  wa shilingi  milioni 96,686,285  atafanya kazi ya Matengenezo  ya  muda maalum barabara  Mtwivila  sekondari na Mwaikasu ndani ya  muda wa  miezi minne na kazi hiyo ni kutengeneza mifereji huku Manispaa imesembea  barabara  hiyo .

Alisema hali ya  barabara  hiyo ilikuwa mbaya   kutokana na kuharibiwa na  Mvua  kubwa  zilizopata  kunyesha  kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu  ambazo zimepelekea  barabara  nyingi  za mji  wa Iringa  kuharibika na  baadhi  kutopitika  kutokana na ubovu  uliopitiliza hali inayosababisha kero  kubwa  kwa  watumiaji  wa  miundo mbinu ya  barabara  hizo.

Mstahiki Meya  Kimbe  alisema katika  zoezi la kuwasainisha mikataba hiyo jumla  makadanrasi 14 walisainishwa na kiasi cha  Shilingi bilioni 1,389,455,041.20 kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo .
Kuwa halmashauri yake imeendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia fedha za mfuko wa barabara.
"Kazi zinazokusudiwa kufanyika ni matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance works) ikihusisha ujenzi wa barabara ya lami ya Frelimo -Muungano (Routine maintenance works) na ujenzi / ukarabati wa madaraja "
Anasema   kuwa mchakato wa kuwapata wakandarasi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ukifanyika kwa mujibu wa sheria ya manunizi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake na kuwa zabuni za ushindani kitaifa zilitangazwa katika magazeti na website za zabuni ya mamlaka ya uthibiti wa manunuzi ya umma hivyo alitaka wakandarasi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Kuwa  kazi zitakazofanywa kwa  mujibu wa mikataba hiyo ni utengenezaji wa barabara ya kiwango cha lami Barabara ya Frelimo,na Muungano pia matengenezo ya kawaida ya barabara za kata za Mtwivila, Nduli, Mlandege, Mshindo, makorongoni, Kitanzini Isakalilo, Mvinjeni, Gangilonga, Ilala, Kitwilu, Ruaha, mkwawa, Mkimbizi, Kihesa na maeneo mengine ya mji wa Iringa. 


Wananchi  wa kata ya Mtwila kwa nyakati  tofauti  walieleza  kusikitishwa na utengenezaji wa barabara   hizo kwa  kiwango cha  chini  kutokana Manispa  kupitisha  greda  pasipo kumwaga kifusi wala  kusindilia barabara   hiyo  hivyo waliomba serikali ya  mkoa  wa Iringa  kuchunguza  matengenezo hayo ya  barabara  ili  kuepusha matumizi mabaya ya  fedha .

Tayari  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  alipata  kutembelea kukagua  barabara  hiyo na  kueleza  kutofurahishwa na matengenezo hayo na  kusema atafika na injinia wa Manispaa ya  Iringa kwa  ukaguzi zaidi  huku akiagiza makandarasi  wote  kuweka vibao vya ujenzi  ili  iwe  rahisi  kujua  nani kafanya  vibaya .

Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Dkt Wiliam Mafwele  alisema kuwa kusudi la Manispaa ni kuweza  kuboresha barabara  zake na  kuona  wananchi hawapati shida tena na usafiri  unaokwami
shwa na ubovu wa barabara .

Kwani  alisema hatua ya halmashauiri yake kusembua  barabara ya Mtwivila  sekondari na nyingine  ni kuwezesha  wananchi  kupata huduma bora ya  usafiri wa daladala .
   

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE