May 22, 2017

MANISPAA YA IRINGA YAFUKUZA KAZI WATUMISHI SITA

Mstahiki  meya wa halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe akiongoza kikao cha baraza la madiwani  kilichofukuza watumishi  sita kwa makosa mbali mbali
Madiwani Manispaa ya  Iringa  wakiwa katika baraza lao
Kikao  cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  kikiendelea  katika  ukumbi wa manispaa
Wakuu  wa Idara  wakifuatilia  kikao  hicho
Madiwani  wa CCM Dolla Nziku na diwani wa Kitanzini  wakifuatilia ajenda  mbali mbali

Diwani wa kata ya Mshndo Ibrahim Ngwada  akihoji  juu ya machinjio kuendelea  kusuasua

Mstahiki  meya  Alex  Kimbe  akisikiliza hoja za wajumbe
Mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa Dkt  Wiliam Mafwele  akijibu hoja za  wajumbe

Aliyekuwa mstahiki meya wa Manispaa ya  Iringa Amani Mwamwindi  akichangia  hoja katika  kikao  hicho
Diwani baraka Kimata akichangia  hoja


Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  akichangia  hoja katika kikao  cha baraza la madiwani

Diwani wa kata ya Kihesa  akichangia hoja na kumpongeza Mwamwindi kwa ushauri mzuri

Naibu  meya wa Manispaa ya  Iringa Bw Lyata  akiwasilisha kazi ya kamati yake

Kikao cha baraza  kikimalizika
kada  wa Chadema na mchambuzi wa siasa mkoani Iringa  David Butinini kulia  akiwa katika kikao hicho
Madiwani  wakipiga kura kuwafukuza kazi  watumishi  6 kwa  utoro


Na MatukiodaimaBlog

BARAZA  la madiwani  la Halmashauri  ya  Manispaa ya  Iringa mkoani Iringa  limewafukuzwa kazi  kwa utoro  kazini watumishi 6 wa Halmashauri  hiyo  na  kumrudisha  kazini mtumishi Lucy Mtafya baada ya  kamati kuchunguza makosa yake yaliyopelekea  kutakiwa  kufukuzwa kazi kuwa hayana ukweli . 

Uamuzi   wa  kuwafukuza kazi watumishi hao ulifikiwa juzi katika  kikao cha  baraza la madiwani ambalo kabla  ya  kukubaliana  kufukuzwa kazi kwa  watumishi hao  watoro liliketi  kama kamati kuwajadili na baadae kurejea  kama  baraza na kupiga kura zilizoamua  watumishi  hao kufukuzwa kazi.

Mstahiki  meya wa halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Alex Kimbe  aliwataja  watumishi  hao  waliofukuza  kazi kuwa ni  Glory Ngowi, Francis Mkenge , Paul Sanga , Anzawe Mvena ,Tumaini Sanga na Mkombozi Gendangenda ambao  wote  walikuwa  watumishi katika   idara  mbali mbali  ndani ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa .

Hata  hivyo  alisema Lucye Mtafya  ambae  alikuwa akifanya kazi  mfuko wa  maendeleo ya  jamii (TASAF ) na  kusimamishwa kazi na uongozi wa  TASAF Taifa  baraza  hilo limemrejesha kazini  baada ya  kufanya uchunguzi dhidi yake na kuona makosa yake hayana  ukweli wowote .

Kimbe  alisema  kuwa halmashauri   hiyo haitakubali  kuendelea  kuwalipa mishahara  watumishi wasiofika kazini na kuwa mfano  ulioonyeshwa kwa  watumishi  hao sita ndio  utakaoendelea  kwa  watumishi  wengine  ambao wanapokea  mshahara wa  serikali bila  kuwajibika kazini .

Katika hatua  nyingine  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa imesema imefanikiwa  kukusanya  shilingi milioni 209,797,248.30   kati ya januari hadi machi  mwaka 2016/17kukonana na  kodi ya ardhi  huku juma ya hati miliki 51 zimetayarishwa na kupelekwa kwa  kamishina wa  ardhi  na michoro 11 ya mipango  miji eneo la Nduli na  kingonzile iliidhinishwa  na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi .

Meya  huyo   aisema  kuwa  katika  kitengo cha upimaji na ramani kazi ya urasimishaji  na uchoraji wa ramani ya makazi 800 eneo la Igumbilo  zimefanyika na kufikia asilimia 95 na jumla ya viwanja 80 vimerudishwa mipaka maeneo mbali mbali ya manispaa ya Iringa .

Aidha  ramani za majengo 120 zimetolea na zimewasilishwa na kupitishwa kwenye kamati  ndogo ya  vibali vya ujenzi  ndani ya manispaa ya Iringa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE