May 31, 2017

MANISPAA YA IRINGA SHIMO HILI NI AIBU KUBWA

Taili  la nyuma la gari hili  likiwa  limepasuka  leo  baada ya  kuingia katika  shimo  hili lililopo  eneo la Mahakama kuu kanda ya  Iringa  jirani kabisa na  nyumba ya mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  barabara  ya  kuelekea  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa ,kweli  hii ni aibu lazima  mhadisi  Manispaa ya Iringa  kutembelea  eneo hili 
Dereva  wa  gari lilopata  tatizo kwa  kupasuka  taili kwenye  shimo akijiandaa kutengeneza  gari lake 
Hii ni aibu kwa  shimo kama  hili usoni mwa  Manispaa kushindwa kufukiwa hata kwa  kifusi  cha kawaida  nipo  tayari  kusomba kifusi kwa toroli  kujitolea  kufukia japo chini ya kiwango iwapo Mhandisi wa Manispaa ya Iringa ataniandikia  barua ya  kuomba  nimsaidie  kufukia aibu  hii .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE