May 5, 2017

MAJAMBAZI WAUA MTU TENA RUFIJI MKOANI PWANI

Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada ya watu wasiojulikana kufika kwake na kutekeleza shambulio hilo.
Marehemu huyo ambaye pia ni mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni baada ya siku tano kuuawa kwa  Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa ni mwanachama wa chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani Rufiji, Musa Nyeresa amethibitisha kuuawa kwa mwanachama huyo kwa kupigwa risasi.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE