May 8, 2017

MAELFU WAHUDHURIA IBADA YA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT MKOANI ARUSHA

    Mmoja wa waliohudhuria ibada hiyo akifarijiwa

                                     Mmoja wa waliohudhuria ibada hiyo akifarijiwa

Maelfu ya watu leo wamejitokeza kuhudhuria ibada ya pamoja kuwaaga wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vicent waliofariki dunia ajalini Jumamosi asubuhi.
Mwandishi wa BBC aliyepo Arusha Aboubakar Famau anasema majeneza 35 yenye miili ya waliofariki yalifikishwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwa ibada ya mwisho ya kuwaaga waliofariki kabla ya kufanyika mazishi sehemu tofauti.

Shughuli nyingi mjini Arusha zilisimama leo na hata maduka na biashara zingine kufungwa huku watu wengi wakifika uwanjani kuhudhuria ibada hiyo.
Baadhi ya watu waliofika kuomboleza walipoteza fahamu hivyo kupewa huduma ya kwanza huku wengine wakikimbizwa hospitalini.
Makamu wa rais Bi Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wakuu serikali waliohudhuria ibada hiyo.

Amevitaka vyombo husika vihakikishe suala la usalama barabarani linapewa kipaumbele.
"Nawaasa madereva kuwa makini wawapo barabarani na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara," amesema.

Waziri wa elimu wa Kenya Dkt Fred Matiang'i, mmoja wa wageni kutoka nje ya Tanzania waliohudhuria ibada hiyo, amewapa pole Watanzania kwa msiba huo.
Manejewa yakiwa kwenye meza maalum
Majeneza yakiwa kwenye meza maalum
"Kenya itaendelea kuwa pamoja nanyi kwenye kipindi hiki kizito cha msiba huu mzito uliowafika. Msiba huu si wa Tanzania peke yake ni wa wote hata kwetu Kenya Rais Kenyatta na mkewe wanawapa pole sana na kuwaombea," amesema.

Rais Magufuli kupitia ujumbe kwenye Twitter, ameelezea, jinsi alivyopatwa na huzuni kutokana na ajali hiyo.

"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha. Tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu," amesema.
Ujumbe wa Magufuli Twitter                           
Majenza yakitolewa kwenye lori
                                     Majeneza yakitolewa kwenye lori na wanajeshi wa JWTZ
Wanafunzi hao wa darasa la saba walifariki dunia pamoja na walimu 2 na dereva wa gari la shule hiyo ya msingi ya Arusha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni.
Wanafunzi watatu walijeruhiwa.

Rais Magufuli, akituma salamu za rambirambi Jumamosi alisema „ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla."

"Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu Wakazi wamejitokeza kwa wingikatika kipindi hiki kigumu."Baadhi ya waliohudhuria ibada hiyo wamezidiwa na huzuni

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE