May 25, 2017

MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA ZIARA YA RAIS TRUMP YAFANYIKA NCHINI UBELGIJI

Waandamanaji BrusselsWaandamanaji Brussels
Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuwasili katika mkutano wa viongozi wa Ulaya na NATO.

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango ambayo baadhi yalikuwa yakisomeka ''Hatumkaribishi Trump''.


Wakati wa kampeni za Urais nchini mwake, Rais Trump aliwakasirisha Wabelgiji wengi kutokana na kuielezea kwake Brussels kama Jahanam.


Awali Rais huyo wa Marekani alikutana na mwenyeji wake mfalme Philippe wa Ubelgiji na malkia Mathilde.


Aliwasili mjini humo akitokea Roma Italia, ambako alikutana na kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE