May 16, 2017

KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA WAMVUTIA WAZIRI JAFO , ASEMA ZAIDI YA TSH MILIONI 239 KUJENGA DARAJA KIWALAMO

naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo aliyetangulia  akitoka  kukagua  ujenzi wa Majengo ya  Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo ,anayefuata ni mbunge wa  Kilolo  Venance Mwamoto
naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo akizungumza na  viongozi wa Kilolo  baada ya  kutembelea  ujenzi wa Hospitali ya  wilaya hiyo wa  pili kushoto ni mhadisi  wa wilaya  hiyo Yahaya Wahabu Nyamuzungu  
Mbunge  Mwamoto  katikati na  mhadisi wa  wilaya  Nyamuzungu  wakimfuatilia  waziri Jafo
naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo akiwafanya  Mwamoto na mhadisi  wilaya ya  Kilolo  kuangua  kicheko wakati  akipongeza kazi nzuri ya ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo
naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo akipokea  taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo
Viongozi  wa wilaya ya  Kilolo  wakimpokea  naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo
Dc Kilolo  Asia Abdalah  akiongozana mbunge  Mwamoto    wakati  wa ziara ya naibu  waziri Tamisemi  leo
naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo akikagua  ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya Kilolo  aliyetangulia ni mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati
Mbunge  Mwamoto  akimshukuru  naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo
Jengo la utawala katika  Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo inayojengwa
Na matukiodaimaBlog
SERIKALI imepongeza kasi kubwa  ya  ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa  mkoani Iringa itakayokamilika kwa kiasi cha  Shilingi bilioni 12 huku akiahidi kuendelea  kutoa ushirikiano mkubwa katika kutatua  changamoto  mbali mbali  zilizopo  wilaya  ya  Kilolo ikiwa ni pamoja na kuwajengea  wananchi wa  daraja la Kiwalamo ambalo tayari imepitisha  kiasi cha shilingi  milioni 239 kwa  ajili ya daraja   hilo.

Akizungumza  leo na   viongozi  wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo  wakati wa ukaguzi wa  ujenzi wa Hospitali ya  wilaya ya  Kilolo ,naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo alisema  kuwa kuhusu  suala la ujenzi wa Hospitali  hiyo  wilaya  ya  Kilolo imeonyesha usimamizi mzuri  kiasi  cha Halmashauri  nyingine ikiwemo ya Buhigwa  kufika  kujifunza  kazi  nzuri  zinazofanywa  wilaya ya  Kilolo.

Alisema  kuwa  katika maeneo  mbali mbali ya  nchi  ambayo yalipata  pesa  pamoja na Halmashauri ya  Kilolo maeneo  yaliyomengi  yanafanya kazi kwa  kusua  suala  ila  kwa  wilaya ya  Kilolo  kazi  inayofanyika  inaleta  matumaini makubwa na ofisi  yake  inapongeza viongozi  wote wa wilaya  hiyo ya  Kilolo kwa  usimamizi mzuri  wa pesa  za miradi .

“Wenzenu  wote waliopewa  pesa  ninyi  Kilolo  mmeenda kwa  kasi kubwa na nzuri na  Buhigwa  walipata  milioni 400 na ninyi  mlipata bilioni 1  ila kazi  mnayofanya ni  nzuri  sana kweli  nimefarijika na nitaendelea  kumshauri mheshimiwa rais  ili  pesa  nyingine  tena  ziweze kuja Kilolo  ili kumalizia ujenzi wa Hospitali  hii “

Jafo  alisema pamoja na   Halmashauri ya  Kilolo kupewa  pesa  za miradi ila tayari  Halmashauri  nyingine  zote  pesa  wamekwisha  pewa  na kuwa  kumekuwepo na mafanikio makubwa  zaidi ya pesa  zilizotolewa kwa ajili ya  miradi mbali mbali kwenye  Halmashauri .

Hata  hivyo  alitaka Halmashauri ya  Kilolo kutolea taarifa  fedha   walizopewa kwa ajili ya kazi hiyo kwa kubainisha  matumizi ya  fedha   hizo  ili kuomba  fedha  nyingine kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali  hiyo .

Akielezea  kuhusu  changamoto ya  daraja la Kiwalamo  alisema  kuwa anapongeza viongozi wa CCM Kilolo  na wana CCM kwa   kujitolea  kuanza  kuchangishana  pesa kwa  ajili ya ujenzi wa daraja hilo japo  tayari  serikali imepitisha  pesa kwa  ajili ya ujenzi  wa daraja la kisasa katika eneo  hilo la mto Kiwalamo .

Hivyo  alimtaka  mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  na mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo kusimamia ujenzi wa daraja  hilo ili  kuepusha  vifo  kwa wananchi wanaotumia  daraja  hilo .

Akijibu maswali ya  wanahabari Kuhusu  changamoto ya  barabara   ya lami katika wilaya ya  Kilolo  kutoka mjini Iringa  hadi Kilolo alisema  kuwa moja kati ya  vipaumbele  za Rais Dkt Magufuli ni kuona  ahadi  zake  zote  zinatekelezwa  na tayari kazi hiyo  imeanza katika maeneo  mbalimbali ya  nchi  na  kuwa imani  yake barabara  hiyo ya Iringa hadi  Kilolo kwa kiwango  cha lami itafanyiwa kati kwani imo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015  -2020 .

 

Huku  akisema kuwa  suala la  kugawasha  wilaya ya  Kilolo kuwa na Halmashauri  mpya linafanyiwa kazi kwani  tayari  wataalam  walifika  kufanya  utafiti na wapo katika uchambuzi wa nyaraka mbali  mbali   kabla ya  kupeleka kwa Rais ambae  ndie  mwenye mamlaka ya mwisho  kama itabidi .

“Napenda  kumshukuru pia mbunge wa Kilolo  Venance  Mwamoto  ambae  amekuwa akilipigia  kelele  suala la  kugawashwa kwa  Halmashauri  ya  Kilolo  ili  kusogeza  huduma kwa  wananchi wote”

Kwa upande wake  mbunge wa Kilolo  Mwamoto  alimpongeza  Rais Dkt Magufuli kwa kupitia wizara ya Tamisemi kwa  kutoa  pesa kwa  ajili ya ujenzi wa Hospitali   hiyo ya  wilaya  kwani alisema  ujenzi wa Hospitali  hiyo utasaidia  kuondoa kero ya  wananchi  kupata   huduma  umbali mkubwa hadi  Hospitali ya llula au Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa.

Alisema  kuwa  wilaya ya Kilolo  ina zaidi ya miaka 10  haijapata  kuwa na Hospitali ya  wilaya  na kutokana na kukosekana kwa  Hospitali  walikuwa  wakilazimika  kutumia gari ya mkurugenzi kubeba  wagonjwa   huku  akitaka uwazi  wa fedha  ziazoingia kwa  ajili ya miradi mbali mbali  uwepo  ili  wananchi  wawe  na  taarifa ya jitihada  zinazofanywa na  serikali yao .

MKuu wa  wilaya ya Kilolo Asia Abdalah  alisema kuwa  kazi nzuri  inayofanyika katika ujenzi wa Hospitali  hiyo ni matunda ya  ziara ya  naibu  waziri  huyo aliyoifanya mwaka jana na  kuwa imani ya  wananchi wa Kilolo  kupiga hatua  zaidi  na  hivyo maagizo yote  ambayo wamepewa  watayasimamia ili wananchi  waweze  kunufaika na serikali yao .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE