May 24, 2017

KAMPUNI YAJITOLEA KUJENGA VYOO SHULE YA MSINGI NDULI

Mkuu wa  shule ya Msingi Nduli akionyesha  ramani  ya shule ya Msingi Nduli
Mkurugenzi wa  kampuni ya Makota  Forest Bharat Bhesania akimwonyesha  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  ramani ya  vyoo  ambavyo kampuni yake itajenga  shule ya Msingi Nduli mjini Iringa
Choo  kinachotumika  sasa  shule ya Msingi  Nduli
Kaimu  mkuu wa wilaya ya Iringa  Asia  Abdalah  akitoa  shukrani kwa kampuni ya makota  Forest  kwa  kujitolea  ujenzi wa choo shule ya Msingi Nduli
kaimu mkuu wa wilaya ya  Iringa Asia Abdalah wa  nne  kushoto akiwa na wadau  mbali mbali
KAMPUNI ya  Makota Forest ya inayojihusisha na  shughuli  za  Kilimo  katika kata ya  Ihimbo  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa imejitolea  kujenga  vyoo vya  kisasa katika  shule ya Msingi  Nduli katika Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa.
 
Akizungumza  wakati wa zoezi la kukabidhiwa  ramani  na BOQ ya  ujenzi wa vyoo  jana  mkurugenzi  wa kampuni  hiyo ya Makota Forest Bharat Bhesania alisema  kuwa kampuni yake imeamua  kusaidia ujenzi huo kufuatia  maombi ya  uongozi wa  shule  hiyo kupitia kwa meneja wa  kiwanja  cha Ndege  Nduli .

Alisema  kuwa  kutokana na shule  hiyo kuwa jirani ya  uwanja wa Ndege  wa mkoa wa Iringa alilipokea  ombi  hilo la ujenzi wa  vyoo  vya kisasa  kutokana na vyoo  vilivyokuwepo kuwa katika hali mbaya zaidi na kutishia usalama wa afya  za wanafunzi  shuleni hapo.

Mkurugenzi  huyo  alisema kutokana na shule  hiyo  wanafunzi  kutokuwa na vyoo  vya kisasa  kampuni yake  imejitolea  kujenga  kwa kasi  kubwa  vyoo  hivyo ambavyo  vitakuwa ni  vyoo  vya kisasa  vinavyoendana na hadhi ya  uwanja  huo wa  Ndege  Nduli na kuwa kazi hiyo itafanyika ndani ya  kipindi  kifupi  zaidi  ili  kuepusha wanafunzi  kupatwa na magonjwa ya milipuko.


Aidha  alisema kuwa kampuni  yake  itaendelea  kuchangia  shughuli mbali mbali za  kimaendeleo ndani ya mkoa  wa Iringa bila kujali kuwa  shughuli zake imekuwa ikizifanyia katika wilaya ya Kilolo.
 
Berthania alisema mbali ya  kusaidia ujenzi  huo wa vyoo matundu  nane  kwenye  shule  hiyo bado kampuni  yake  amepata kutoa  msaada  wa  bati  100 pamoja na madawati  20 kwa ajili ya  kuunga  mkono  serikali ya  wilaya  ya  Kilolo ya ujenzi  wa  vyumba vya madarasa  pia  kuunga mkono jitihada za  Rais Dkt John Magufuli la  kumaliza kero ya madawati mashuleni .
 
 " Sisi  kama  wawekezaji  tunaowajibu  wa  kuunga  mkono  shughuli  zote za  kimaendeleo  zinazoendelea  katika  maeneo  yetu ....nimekuwa nikisaidia shughuli  nyingi sana na sichoki  kuendelea  kusaidia "

   Kwa  upande  wake mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo ya Kilolo Asia Abdalah ambae  ni kaimu mkuu wa wilaya ya Iringa  alimpongeza mkurugenzi mtendaji  wa kampuni Makota Ferest  kwa  kuendelea  kuunga mkono jitihada mbali mbali  za kijamii katika  mkoa wa Iringa 
 
Alisema   kuwa msaada wa mwekezaji   wa kampuni ya Makota  Forest  ni  mwanzo wa  wadau  wengine  kujitokeza  kusaidia  katika maeneo yao  huku  akitaka  uongozi wa  shule  hiyo ya Nduli kuweka mazingira  safi ya  shule  hiyo  kwa kupanda  miti na maua kwani ni shule  iliyopo machoni mwa watu wa mataifa mbali mbali .
 
Alisema  kuwa  jitihada  zinazofanywa na viongozi wa  mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza  katika  kuwaletea  wananchi maendeleo ni  jitihada  ambazo zinapaswa   kuungwa mkono na  wadau  wote wa maendeleo  ndani ya  mkoa  huo  na  waliopo  nje ya  mkoa .


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE