May 2, 2017

JESCA MSAMBATAVANGU AFIKISHWA MAHAKAMANI ,ATOLEWA KWA DHAMANA

'Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Dkt   Jesca Msambatavangu  akiingia mahabusu mahakama ya  Iringa kusubiri taratibu  za dhamana baada ya kuachiwa kwa  dhamana na makhakama ya   hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa  wa Iringa leo  alipofikishwa mahakamani  hapo kwa kosa jinai namba 65 la mwaka 2017 aliloshitakiwa kwa  kumpiga Neema Nyongole  mkazi wa  Kibwabwa mjini Iringa ,kesi hiyo  itaendelea tena  tarehe  1/6/2017  (picha na Francis Godwin wa matukiodaimaBlog )
Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Dkt   Jesca Msambatavangu  akifikishwa katika mahakama ya  hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa  wa Iringa kusomewa  shitaka  lake la   jinai namba 65 la mwaka 2017 aliloshitakiwa kwa  kumpiga Neema Nyongole  mkazi wa  Kibwabwa mjini Iringa ,mahakama hiyo  imemwachia kwa  dhamana hadi tarehe  1/6/2017 kesi  hiyo  itakapo tajwe  tena  mahakamani hapo baada ya  upelelezi wake   kuendelea(picha na Francis Godwin matukiodaimaBlog )
Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Dkt   Jesca Msambatavangu  akiwa katika mahakama ya  hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa  wa Iringa kusomewa  shitaka  lake la   jinai namba 65 la mwaka 2017 aliloshitakiwa kwa  kumpiga Neema Nyongole  mkazi wa  Kibwabwa mjini Iringa ,mahakama hiyo  imemwachia kwa  dhamana hadi tarehe  1/6/2017 kesi  hiyo  itakapo tajwe  tena  mahakamani hapo baada ya  upelelezi wake   kuendelea (picha na Francis Godwin matukiodaimaBlog )

 
 Na MatukiodaimaBlog
MAHAKAMA  ya hakimu mfawidhi mkoa  wa  Iringa  imemwachia  kwa dhamana aliyekuwa  mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Dkt Jesca Msambatavangu (41)aliyeshitakiwa kwa  kesi yake ya  jinai namba 65 ya mwaka  2017.

Akisoma shitaka   hilo  leo  mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Iringa jana  mwanasheria  upande  wa jamhuri Alex  Mwita  alisema  kuwa Msambatavangu anadaiwa   kumshambulia Neema Nyongole mkazi  wa Kibwabwa  katika Manispaa ya  Iringa Februari 17 mwaka huu  katika  eneo la Kibwabwa  kosa   hilo ambalo ni kinyume na  kifungu  cha  seria kanuni ya  adhabu sura namba 16 marejeo  mwaka 2002.

Alisema upalelezi  wa  kesi hiyo  unaendelea na kutokana na  kosa  hilo upande wa  jamhuri  hauna pingamizi ya  dhamana kwa  mtuhumiwa   huyo .

Dkt  Msambatavangu  alikana kuhusika na kosa  hilo huku  hakimu anayesikiliza  kesi hiyo David Ngunyale alisema  kuwa  dhamana kwa  mshitakiwa  ipo  wazi na  kumtaka kutimiza masharti  ya  dhamana ya kuwa na  wadhamini  wawili  waamini  ambao  kila mmoja atasaini dhamana ya shilingi milioni 1 .

Idadi ya  wadhamini waliofika mahakamani  hapo  waliweza kutimiza masharti hayo na  hivyo  kufanikiwa kutoka kwa  dhamana  hadi kesi  hiyo  itakakapo tajwa  tena mahakamani  hapo June 1 mwaka huu .

Dkt Msambatavangu  anayetetewa na mawakili  wawili  Alfred Mwakingwe na Jackson Chaula alifikishwa mahakamani hapo  majira ya saa 4;8  asubuhi kwa  gari  la polisi Toyota Land Cruiser akiwa amekaa siti ya  mbele  huku  nyuma kukiwa na ulinzi  mkali  wa askari  wa  kikosi cha FFU na  kuingizwa mahabusu ya mahakama   kwa  muda kabla ya  kufikishwa mahakamani .

Idadi   kubwa ya  wananchi walifika katika mahakama  hiyo  kusikiliza kesi  hiyo  wakiwemo viongozi wa Chama  cha Demokrasia na maendeleo  (Chadema)  wakiongozwa na mwenyekiti wake wa  wilaya  Frank Nyalusi , Mstahiki meya wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe ,naibu  meya  wake na watu mbali mbali huku zaidi ya watu sita  walikuwa na barua  za  dhamana na muda  wote  akiwa mhakamani  hapo Dkt Msambatavangu  alikuwa mwenye sura  ya furaha .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE