May 3, 2017

JACK PEMBA AKAMATWA KWA UTAKATISHAJI WA HELA UGANDA


. Mtanzania anayevuma kwenye mitandao ya kijamii kutokana na matanuzi ya fedha, Jack Pemba yuko mikononi mwa vyombo vya dola akichunguzwa kutokana na tuhuma za utakatishaji wa fedha.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Asan Kasingye amethibitisha kukamatwa kwa Mtanzania huyo na kwamba alikamatwa wakati akijaribu kuondoka nchini humo.
“Alikamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe wakati akijaribu kuondoka nchini,” amesema msemaji huyo na  kuwa uchunguzi huo unafanywa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya askari wa Tanzania na Uganda.
Pemba ambaye hivi karibuni picha zake zilisambaa kwenye mitandao akigawa fedha kwenye matamasha ya muziki amekuwa akitiliwa shaka kuhusu chanzo cha utajiri wake.
Hivi karibuni alihusishwa katika sakata moja la linalohusu madini ya dhahabu yenye thamani ya mabilioni ya shilingi.
Polisi nchini Uganda imekanusha ripoti kuwa imekuwa ikimkingia mkono mfanyabiashara huyo.
Gazeti moja linalochapishwa mtandaoni liliripoti kuhusu kufutwa kwa kesi iliyokuwa ikimkabili Pemba ya kujihusisha na biashara ya dhahabu bandia. Gazeti hilo lilisema kesi hiyo iliyeyuka kimyakimya baada  kigogo wa polisi kuamuru iondolewe.
Baada ya kutoweka nchini kwa muda, Pemba aliyekuwa akiishi Uingereza alihamishia makazi yake Kampala nchini Uganda

Share this story

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE