May 2, 2017

INJINIA MPANGALA ASAIDIA SHULE YA MSINGI NA UFUNDI KALENGA ,SHULE ALIYOSOMA

Dastani Mpangala kushoto akikabidhi msaada  wa  chelehani mbili  zilizotolewa na mkurugenzi wa Taifa  wa miradi ya maji kanisa la Romani Cathoric  injinia Godfrey Mpangala kwa  shule ya Msingi na ufundi Kalenga mkoani Iringa shule  ambayo injinia Mpangala  alisoma kuanzia  darasa la kwanza na la tatu mwaka 1977-1979 alipohama ,kutoka kulia ni mjumbe wa  bodi ya  shule Shakra Ugali , mwalimu Joseph Shubi , mwalimu wa kitengo cha ufundi  shuleni hapo Perida Mwihava ,Ibrahim Nzalawae  mjumbe wa  bodi ya  shule na Ignas Kahovela mjumbe  pia
Wajumbe wa  bodi ya  shule ya msingi na ufundi Kalenga  wakipokea taarifa ya msaada wa chelehani  zilizotolewa na injinia Mpangala
Wajumbe walimu  wakipongeza  msaada  huo
Wanafunzi  wakisaidia  kubeba  chelehani  zilizotolewa msaada

Na MatukiodaimaBLog

Akikabidhi msaada  huo  leo    kwa uongozi  wa  shule  hiyo na wajumbe wa kamati ya shule kwa niaba ya Mpangala ,mzazi wa kijana   huyo ,baba mzazi wa Mpangala  Dastan Mpangala  alisema  kuwa baada ya  kutembelea  shule   hiyo  alishuhudia changamoto mbali mbali  ikiwemo ya  uchakavu wa  majengo na  uhaba wa  vyerehani  kwa  wanafunzi wa  darasa ya  ufundi .

Hivyo  alisema   kutokana na maombi ya  walimu wa  shule  hiyo  alikubali  kujitolea  kununuachelehani  hivyo  ili  kuwasaidia  wanafunzi  hao wa  darasa la ufundi ambao  wengi  wao ni  wale  ambao  walikosa  sifa ya kuendelea na masomo ya  sekondari.

Alisema  kuwa  alipata  kusoma  shule   hiyo kati ya  mwaka 1977 -1979  alipohama  akiwa  darasa la  tatu na  kuwa  yupo tayari  kuendelea  kusaidia  zaidi  kutatua  changamoto mbali mbali  shuleni hapo  kulingana na uwezo  wake .

Akishukuru  kwa  niaba ya  mkuu  wa  shule  ya msingi  Kalenga mwalimu  wa  darasa  la ufundi  Perida Mwihava  alisema  kuwa msaada  huo utapunguza changamoto ya  upungufu wa  vyerehani katika  darasa  hilo .

Alisema  kuwa  awali  darasa  hilo  liliandikisha  wanafunzi  15  kwa  mwaka  huu  ila  kutokana na uhaba wa  vitendea kazi  baadhi yao  waliacha masomo  na  kubakia na  wanafunzi 7 pekee ila  kuongezewa  vifaa hivyo  kutaongeza  idadi ya  wanafunzi  zaidi .

Hata   hivyo kumekuwepo kwa  jitihada mbali mbali za  kuomba misaada  maeneo mbali mbali na  kuwa tayari  wadau mbali mbali  wamefika  kusaidia  kama mbunge wa  viti maaalum mkoa wa Iringa (CCM) Zainab Mwamwindi na  shirika la UNCEF ambao  ambao  walisaidia chelehani  6 .

Alisema  kuwa  kituo ni  maalum kwa ajili ya  vijana  waliokosa  sifa ya  kujiunga na  sekondari  wasichana na  wavulana  ili  kuwaepusha na kushinda  vijiweni ama  kujihusisha na  vitendo vya kihuni kama matumizi ya  dawa  za  kulevya na ukahaba .

Pia  alisema  kupitia  diwani  wao wa  viti maalum ameweza  kupigania shule   hiyo  kupata kiasi cha shilingi  milioni 241 kwa  ajili ya  ukarabati wa   majengo ya  shule   hiyo ambayo yamechakaa sana.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE