May 31, 2017

IGP SIRRO ATANGAZA ZAWADI YA MILIONI 10,MAUAJI YA KIBITI


 Mkuu mpya wa majeshi, IGP Simon Sirro amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo,   na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.
Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.
“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema
BRIEFING
 Oktoba 2016
Kadhalika, Oktoba mwaka jana aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Ally Milandu aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wanne, waliompiga risasi mbili.
 Novemba, 2016
Novemba mwaka jana, wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi.
 Januari 2017
Januari mwaka huu, katika kijiji cha Nyambunda, kitongoji cha Mkwandara, watu wasiofahamika walimuua mfanyabiashara, Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake.
 Februari 2017
Tukio jingine ni lile la Februari 3, mwaka huu ambapo majambazi walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, ambaye alifanikiwa kuwatoroka.
Hata hivyo majambazi hayo yalipomkosa, yalirejea na kumwaga mafuta, kisha kuichoma moto nyumba yake.
 Februari 24
Februari 24 mwaka huu, majambazi hayo yalimuua ofisa upelelezi, wilaya hiyo, Peter Kubezya na maofisa maliasili wawili.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE