May 28, 2017

HALMASHAURI YA IRINGA KUWACHUKULIA HATUA WANAOCHAFUA MAZINGIRA

Mkurugenzi  wa Halmashauri ya  Iringa  vijijini Robart Masunnya  akiwajibika  kufanya  usafi  nje ya  ofisa  yake na  wanafakazi  wenzake  jana  wakati wa utekelezaji wa agizo la Rais  Dkt  John Magufuli  la  usafi  kila jumamosi ya mwisho wa  mwezi
Watumishi wa Halmashauri ya  Iringa wakiwa katika zoezi la usafi 
Watumishi wa Halmashauri ya  Iringa  wakiwajibika  kufanya  usafi  kuzunguka  ofisi ya  Halmashauri  hiyo  jana 
Afisa afya  wa Halmashauri ya  Iringa  vijijini Samwel Obeni  kushoto  akishiriki  usafi 
Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya  Iringa Robart Masunya  kulia  akiwa na wakuu wake wa  idara  wakifanya  usafi  nje ya  jengo la Halmashauri  hiyo 
HALMASHAURI  ya  wilaya ya  Iringa  vijijini mkoani  Iringa  imesema  itaanza  utaratibu wa  kuwapa motisha  wananchi  watakaosaidia kuwakamata  watu  wanaochafua  mazingira  ovyo .

Mwanasheria  wa Halmashauri  hiyo  Kissah  Mbilla  alisema hayo  jana wakati  wa utekelezaji wa agizo la Rais Dkt  John Magufuli la usafi wa mwisho wa  mwezi mara  baada ya  kukamilika kwa zoezi hilo la usafi  katika  ofisi  za Halmashauri  ya  wilaya  hiyo kata ya Ngangilonga  mjini Iringa .

Alisema  kuwa  Halmashauri  hiyo  inayo  sheria  ndogo   kwa  watu  wanaochafua mazingira  ovyo na  kuwa  upo  utaratibu wa  kutoza faini  kiasi cha shilingi 20,000 na  kati ya  pesa  hiyo  kiasi cha shilingi 10,000 hupewa mwananchi atakayefanikisha  kumkamata  mchafuzi wa Mazingira .

Mkurugenzi  wa Halmashauri  hiyo Robart Masunya alisema kuwa wanaendelea  kutekeleza  agizo la Rais la kufanya  usafi  kila juma la mwisho wa mwezi pia  kutekeleza  agizo la makamu wa Rais Samia  Suluhu Hassan la kufanya mazoezi hivyo Halmashauri  hiyo  itahakikisha  inaendelea  kuweka mazingira  safi kwa  kushirikiana na wananchi wa Halmashauri  hiyo.

Aidha  alisema  kuwa katika  Halmashauri  hiyo kumekuwepo na machimbo ya  dhahabu katika  eneo la Nykavangala  na  hivyo  kuwataka wananchi kutunza mazingira na kuepuka  kukata  miti  ovyo  wala kutupa takataka ovyo katika maeneo yao .

Alisema kuwa tayari  Halmashauri  hiyo imepata  kuwapa elimu  mbali mbali  na hivyo  wanamatumaini kuwa  suala la usafi litaendelea  kuboreshwa katika maeneo  yote ya uchimbaji .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE