May 22, 2017

DC KILOLO AMWAKILISHA RC MAZOEZI SAMORA ,ATAKA WANANCHI KUSHIRIKI ULINZI

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akiongoza mazoezi ya viongo  uwanja wa Samora kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
wakazi  Iringa wakiwa katika mazoezi ya  viungo uwanja wa Samora
Aliyekuwa  mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza kulia na mkuu wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam wakishiriki mazoezi
SERIKALI  mkoa wa Iringa  imewataka wananchi wa mkoa  huo kujitokeza katika mazoezi ya  viungo  ili  kuepukana na magonjwa  yasiyo ambukiza .

Pamoja na kushiriki mazoezi hayo yanayofanyika kila jumamosi bado   serikali imewataka wananchi  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa  kuwafichua  waharifu .

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ,mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  wakati wa  mazoezi ya  viongo jumamosi  hii alisema kuwa suala la mazoezi ya  viungo kwa  wananchi litasaidia kuwaepusha na matumizi ya  fedha kwa  kutibu magonjwa hayo yasiyoambukizwa ambayo  husababishwa na kutofanya mazoezi .

Hivyo  alisema kuwa  ni vema kila wilaya kuendeleza mazoezi hayo kama yalivyoasisiwa na makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na  kuendelezwa na mkuu wa mkoa wa Iringa mama Masenza .

Alisema kuwa  mkoa wa Iringa toka  makamu  wa rais aaagize watanzania  wote  kushiriki katika mazoezi kila jumamosi  mmoja kwa  kila mwezi  mkoa huo  umekuwa ukifanya mazoezi  kwa  jumamosi tatu  za  mwezi na jumamosi ya mwisho wa mwezi  ni kwa ajili ya siku ya Rais Dkt John Magufuli ya  kufanya  usafi .

Akielezea  kuhusu suala la ulinzi na usalama  alitaka  kila mwananchi wa mkoa wa Iringa  kuwa mlinzi wa mkoa kwa  kutoa taarifa za uharifu na waharifu kwa  vyombo  vinavyohusika ili  kuufanya mkoa  huo kuwa ni mkoa salama usio na matukio ya uharifu .

Kuhusu vita  ya dawa za kulevya  alitaka vijana kuachana na matumizi ya dawa  hizo na badala yake  kuwafichua  wote  wanaojihusisha na biashara  ya dawa za  kulevya .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE