May 10, 2017

DC KILOLO AAGIZA SHULE KUTENGENEZA UWANJA WA MICHEZO

Wanafunzi wa  shule ya Msingi Mlowa  Kilolo  wakiwa katika michezo ,shule   hiyo haina  uwanja  wa  michezo hivyo  hulazimika  kucheza  vichakani na huchanganyika wa kike na  wa kiume  kucheza mpira wa  miguu
Mchezaji wa kiume  akiwa chini baada ya  kukatwa  chenga  kali na mchezaji wa  kike
Wachezaji  wakiwania mpira
Mwanafunzi huyo  akijaribu  kufunga goli
Mwanafunzi wa kike shule ya Msingi Mlowa akikimbiza mpira  baada ya  kutoka nao kwenye vichaka
Wanafunzi wa  shule ya msingi Mlowa wilaya ya  Kilolo  wakiwa  wamechanganyika kucheza mpira wa miguu kutokana na uhaba wa kiwanja cha michezo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  akitazama mpira  unaotumiwa na  wanafunzi wa   shule ya  msingi Mlowa kata ya Mahenge 
Na MatukiodaimaBlog 
 
KUTOKANA  na wanafunzi  wa  kiume na wa kike kutumia kiwanja  kimoja  kibovu kwa  ajili ya michezo shuleni hapo ,serikali ya wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  imeiagiza kamati ya  shule ya msingi Mlowa  kata ya  Mahenge kuhakikisha inatengeneza viwanja  vya michezo kwa  wanafunzi.

Agizo  hilo  limetolewa na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah jana  wakati wa  ziara  yake ya kukagua miundombinu ya shule  za  msingi zilizopo  kata ya Mahenge .

Mkuu  huyo wa  wilaya  alifikia hatua   hiyo  baada ya  kushuhudia  wanafunzi  wakicheza katika  kiwanja  hicho  kibovu ambacho kina vichaka katikati na  wanafunzi hao  kukosa vifaa vya michezo ,kuwa  akiwa mkuu  wa  wilaya  hiyo hajapendezwa  kuona  shule  hiyo haina hata  kiwanja  kimoja  cha  michezo .

" Naomba  kuwaagiza kamati ya  shule  kushughulikia kero ya  viwanja  vya  michezo katika  shule  hii maana  wanafunzi  wanahaki  ya  kuwa na  vifaa vya  michezo vikiwemo  viwanja  vyenye sifa  za  michezo "

Hivyo  alimtaka  diwani wa kata  hiyo Shera  Ngailo akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata  hiyo  kusimamia utengenezaji wa viwanja  vyenye  vipimo  vya michezo kwa  kushirikiana na kamati ya  shule   hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya  shule  hiyo Malick Wilson alisema  kuwa tatizo kubwa lililopelekea  shule  hiyo  kukosa  uwanja  wa michezo ni kutokana na eneo hilo  kuzungukwa na milima pamoja na mawe  mengi  japo  alisema eneo la kutosha  uwanja  mmoja wa  michezo  lipo  ila lipo juu ya mlima.

Afisa  mtendaji wa  kijiji  cha Mahenge  MUrady Nchimbi na  diwani wa kata ya Mahenge  Shera  Ngailo  walisema  wataanza mchakato wa  kutafuta  wadau kwa  ajili ya  kushughulikia kero ya  uwanja wa  michezo shuleni hapo .

Wanafunzi wasichana na  wavulana katika  shule   hiyo  wamekuwa  wakilazimika kutumia uwanja  mmoja  na mpira  mmoja  kucheza  pamoja  mpira wa miguu ama  mpira  wa  mikono kutokana na uhaba wa vifaa vya  michezo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE