May 28, 2017

DC KASESELA APIGA STOP UCHIMBAJI HATARISHI WA MADINI NYAKAVANGALA , ATANGAZA KUMSAKA MAKAMU MWENYEKITI BAVICHA TAIFA

Baadhi ya  migodi  ya  dhahabu  kijiji  cha Nyakavangala  Iringa  iliyofungiwa  kwa  hofu ya  kuhatarisha maisha ya  wachimbaji  hao 
Dc  Iringa  Richard  Kasesela  akisaidia  kuwavuta  wachimbaji  wadogo wadogo  mgodini  kabla ya  kuzuia  uchimbaji katika  migodi  zaidi ya 10  kuendelea  na uchimbaji jana 
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akizungumza na wachimbaji  wadogo  wadogo  wa madini  eneo la Nyakavangala 
Baadhi ya  wachimbaji  wadogo  wadogo akiwemo  dereva Taxi mjini Iringa Brawn wakimsikiliza mkuu wa  wilaya 
Wachimbaji  wakiendelea na uchimbaji 
Katibu  tarafa  wa Isimani Thomas Mnyinga  akitambulisha  viongozi 
Mwanahabari  Happy Matanji  akitumia  fursa  za  machimbo ya  Nyakavangala 
Machimbo  ya  Nyakavangala  yakikaguliwa 
Nyakavangala  fursa  nje  nje 

                                             Na MatukiodaimaBlog 
SERIKALI  wilaya ya  Iringa  mkoani  Iringa imewazuia  wachimbaji wa  madini  ya  dhahabu wadogo   waliovamia  eneo ya Nyakivangala tarafa ya  Isimani  wilayani Iringa kuendelea  na uchimbaji  katika  migodi zaidi ya 10  ambayo  inatishia  usalama  wa maisha  ya  wachimbaji hao hadi itakapofanyiwa uboreshaji wa  kiusalama .

Huku  ikitangaza  kumsaka makamu  mwenyekiti wa baraza la  vijana wa  chama cha  Demokrasia na maendeleo Chadema ( BAVICHA) Patrick Ole Sosopi kwa  kudaiwa  kutoa  maneo ya  uchochezi  kwa  wachimbaji  hao dhidi ya  serikali .

Akizungumza na  wachimbaji hao jana mkuu wa wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela  alisema  kuwa  serikali  migodi hiyo ambayo imesimamishwa  kuendelea na  uchimbaji  huo ni  ile  ambayo  wachimbaji  wake  wameshindwa  kuiboresha kwa  kujengea miti  pembeni  kwa  ajili ya  kuzuia migodi hiyo kuporomoka  na  ile  ambayo ipo  katika  hali ya  hatari  kwa  usalama  wake .

Hivyo  alitaka  wamiliki wa  migodi hiyo  kuondoa  mchanga  wao wa  Makinikia ya Dhahabu na baada ya  kumaliza  kutoa mchanga  huo  basi  kusitisha  uchimbaji   huo  ili  kupisha uboreshaji wa  migodi hiyo kabla ya  kuendelea na uchimbaji  huo katika mazingira  yanayotishia  usalama  wa maisha  yao.

" Kuanzia  leo hii  natangaza  kusitisha  shughuli  zote za  uchimbaji wa madini  katika  migodi  hii ambayo  kamati yangu ya  ulinzi na usalama  imetembelea  na kuona  ipo  kwenye  hatari  ya  usalama wa maisha  ya  wachimbaji  hao  wanaoendelea na shughuli za  uchimbaji .....tunafanya  hivyo  kwa  usalama  wenu kwani iwapo  itatokea mmoja  wenu amepoteza maisha katika  mgodi huu  basi  wote mtatakiwa  kuondoka  eneo hilo na mgodi  wote  kufungwa "

Pia  mkuu  huyo  wa wilaya  aliwataka  wachimbaji hao  kuendelea  kuifanya kazi hiyo  kwa  kuzingatia usalama  wao  na kuhakikisha  wanaweka  mbele  suala  la usafi  kwa  kila  palipo na mashimo  20  kuwa na choo kwa  ajili ya  kutumia  wachimbaji hao  badala ya  kuendelea  kujisaidia  ovyo .

Kasesela  alisema  kuwa  lazima kila mchimbaji  kuhakikisha  eneo  analofanyia kazi  lipo  kwenye  hali  nzuri ya  usafi na  kuepuka kutupa taka  ovyo ama kutumia dawa  za  kulevya  wakati  wakiwa  kwenye shughuli  hizo za uchimbaji na kuliagiza  jeshi la  polisi  kufanya misako ya mara kwa mara  eneo hilo  ili  wale  wote  wanaofanya  biashara ya  dawa za  kulevya  kuchukuliwa hatua kali.

Kuhusu  wachimbaji hao wasio na leseni  ya uchimbaji  mkuu  huyo wa  wilaya  aliwataka  wachimbaji  hao  kuhakikisha  wanafanya shughuli  hiyo  kwa kuzingatia sheria na kanuni  za  nchi  kwa  kila mmoja  kuwa na leseni na  si  vinginevyo.

Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kupitia kamishina  wa madini nyanda za  juu kusini wale  wote  walioomba  leseni za  uchimbaji hadi tarehe  kumi ya  mwezi ujao watakuwa  wamepatiwa  leseni  za uchimbaji  eneo hilo.

Wakati  huo  huo  mkuu  huyo  wa  wilaya  ya  Iringa amewataka  wanasiasa  kuacha  kuwachochea hao  kuvunja  sheria  za  nchini kwa kuwazuia  kulipa ushuru  kwani kufanya  hivyo ni  kwenda  kinyume na sheria  za  nchi .

Alisema  kuwa kitendo  kilichofanywa na makamu  mwenyekiti wa BAVITA Taifa   kufika  eneo hilo na  kukusanya  wachimbaji kuwazuia  kulipa ushuru  ni  kosa hivyo   serikali  imeagiza  jeshi la polisi  mkoa wa Iringa  kumtafuta  mwenyekiti  huyo na  kumfikisha  mahakamani kwa kauli  zake za  uchochezi  dhidi ya  serikali  pamoja na kuzuia  wachimbaji hao  kulipa  ushuru .

"Tunaendelea  kumsaka  kwani  nasikia  amekimbilia  Dodoma  ila  tutaendelea  kumtafuta  popote  alipo na tukimpata  tutamfikisha mahakamani "

Diwani  wa kata ya Malenga  Makali  Franzisca  Kalinga  alisema  kuwa  kutokana idadi ya  wananchi katika kata  yake  imezidi  kuongezeka na  kuwa  kasi ya  uchimbaji  imeendelea  kunufaisha kata  hiyo  kimapato ukilinganisha na  awali .

Kalinga  alisema  tayari  uongozi wa  kijiji  hicho umefanya mchakato  wa kunufaika na uchimbaji  huo  kupitia kwa mmoja kati ya  wachimbaji ambae wamekwisha  kaa naye Thomas Masuka  kwa  ajili ya  kusaidia kijiji  hicho kama   mdau wa maendeleo kwenye  kijiji cha Nykavangala na kata  hiyo ya Malenga Mkalali 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE