May 18, 2017

DARAJA YA RELI MTO RUVU LAHARIBIKA SAFARI YA TRENI ZASITISHWA

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

KUSIMAMISHWA HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

Uongozi  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusimamishwa huduma ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na Ruvu junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  ya kusitisha huduma kwa muda treni ya abiria ya deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi kwenda Kigoma, imefutwa na abiria wametakliwa wafike stesheni ili warejeshewe fedha zao za nauli.

Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kufanya tathmini na kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundo mbinu husika likiwemo daraja la Ruvu.

Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia ya reli  kati ya Dar es Salaam na Morogoro  itakapofunguliwa tena.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kampuni ya Reli Tanzania(TRL),
Mei 18, 2017
DAR ES SALAAM

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE