May 4, 2017

CATHERINE RUGE ATEULIWA KUWA MBUNGE WA TANZANIA

DSC_0428
KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikaochake cha tarehe 04 Mei, 2017imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge kuwa Mbunge wa VitiMaalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujazanafasiiliyoachwawazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweponafasiwazi ya Mbunge wa VitiMaalumkupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwaMbunge wa VitiMaalumMhe. Dkt. Elly Marko Machakufarikiduniana hivyo kuweponafasiwazi.
Imetolewaleo tarehe 04 Mei, 2017 na:-
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE