May 24, 2017

ALICHOKIANDIKA MTANGAZAJI WA EBONY FM, KEVIN LAMECK KWENYE SIKU YAKE YA KUZALIWA
NINAPOKUMBUKA MIAKA KADHAA YA KUZALIWA HII LEO...
Maalumu kwa Familia na jamaa.

Ilikuwa tarehe 24th May 199, ilikuwa siku ambayo familia ya Mr & Mrs Raymond Lameck walipotunukiwa na Mungu zawadi ya mtoto wa kiume aliye kifunguaMimba. Najaribu kuvuta hisia zangu juu ya furaha waliokuwa nao vijana hawa wa enzi zile kwa kufanikiwa kumpata mtoto mwenye afya njema na ambaye alipofinywa kwenye kisigino cha mguu wake alilia mara tatu kuonyesha kwamba ni mwanaume rijali.

Mtoto huyu siku ya leo anatimiza karibia robo Karne tangu alipozaliwa. Ni kipindi kirefu sana kwa maisha ya mwanadamu wa siku hizi, lakini shukrani za pekee na za dhati zimwendee mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kuwa mlinzi kwa magumu mengi ambayo nimekuwa nikiyapitia kwenye maisha ya kila siku.

Mama yangu mpendwa na baba yangu Kipenzi, hadi leo hii mmekuwa viongozi na walimu wazuri sana kwangu na kila nikaapo na ninyi nahisi nimekaa kwenye kitovu cha elimu. Neno lenu moja kwangu laweza kuwa na nguvu zaidi ya maneno elfu moja niliyowahi kusikia hapa duniani. Nasaha zako kwangu ni zaidi ya elimu niliyoipata shuleni.

Kadhalika pia nisema ahsante kwa kila mtu aliyeyagusa maisha yangu kwa namna moja ama nyingine,mtaani,kazini na kwingineko.

Kubwa ni kuishukuru Familia ya EbonyFm pia imekua familia bora kwangu,yenye kulea na kufundisha na kuelekeza,Maboss na hata wafanyakazi wenzangu naamini mmekuwa msingi katika maisha yangu ya sasa.

Kadhalika wale wanaopenda ninachokifanya na hata kukosoa niyafanyayo,mmekua chachu ya mimi pia kuendelea kusafiri kuzifuata ndoto za mtima wangu na fikra zilizogubika moyoni mwangu.

Nina ndugu pia na wadogo zangu kadhaa,naamini sapoti na msaada na sala zao zimekua na majibu mengi juu yangu.

Kubwa kwa leo ni kuwaombea Afya njema na baraka zake Mungu,zikaendelee kuwa juu yenu.Furaha ya maisha iwe sehemu ya baraka za Mungu kila Uchao.

Mungu aendelee kuwa nasi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE