April 24, 2017

WIKI YA CHANJO DUNIANI , MKOA WA IRINGA WAJIVUNIA KUFANYA VIZURI

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza (kushoto)  akitoa  chanjo kwa  mtoto  Agnes Salila  wa Msisina  kata ya  Nduli  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa   wakati wa uzinduzi wa zoezi la  wiki moja la utoaji chanjo Duniani ambapo kwa  mkoa wa Iringa  limefanyika kata ya  Nduli

Wananchi  wakimsikiliza  mkuu wa  mkoa wa Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza na  viongozi  mbali  mbali  wakifuatilia  ngoma  ya  asili ya  Kihehe leo
Wakazi wa Msisina kata ya  Nduli  wakiwa katika zoezi la uzinduzi wa  wiki  moja ya Chanjo
Wasanii  wa ngoma ya  asili ya  kihehe  Msisina  wakicheza ngoma hiyo ya njuga
Mratibu wa Chanjo  mkoa wa Iringa Dkt Nafari Mwalongo  atosama tarifa ya mkoa juu ya  chanjo
Mratibu wa chanjo  mkoa wa Iringa Dkt Mwalongo  akimpata nakala ya  taarifa yake  mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa  kulia
Mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa  akishukuru kwa hotuba ya mgeni rasmi mkuu wa  mkoa wa Iringa leo
WAKATI  wiki ya chanjo duniani  imeanza  leo  mkoa  wa  Iringa  umejipongeza  kwa   kwa utekelezaji wa zoezi hilo kwa mwaka 2016 baada ya watoto  35,040 sawa na asilimia 94 walipatiwa chanjo.
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza aliyasema hayo   wakati wa  uzinduzi wa zoezi la alipozungumza na  wananchi wa Msisina kata ya Nduli Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ,kuwa mafanikio haya ni zaidi ya malengo yaliyowekwa  kitaifa ya kuhakikisha kila Mkoa unafikia  uchanjaji zaidi ya asilimia 90.


"Ninachukua nafasi hii kwanza  kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya pia naipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mpangilio mzuri wa shughuli hii Siku hii ni muhimu na tunaithamini sana na ni matumaini yangu itaendelea kuadhimishwa kila mwaka, kwa makusudi ya    kuhamasisha na kuelimisha jamii  na wadau mbalimbali juu ya harakati za kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo nchini"

Alisema  kuwa  Tanzania inaungana na nchi  zingine katika kuadhimisha wiki ya chanjo duniani tarehe 24 hadi 30 Aprili, 2017; madhumuni ya Wiki hii ni kuhamasisha na kuelimisha  jamii kuhusu umuhimu wa huduma za chanjo katika kukinga maradhi mbalimbali yanayozuilika kwa chanjo.
 
"Mimi binafsi nimeguswa sana na ujumbe wa   Maadhimisho ya mwaka huu, unaosema: “Chanjo Hukinga kila mtu, pata Chanjo      na       Kauli mbiu ambayo ni     “Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye Afya”. hili limekuwa lengo la serikali kwa miaka mingi sasa"
Mkuu  huyo wa  mkoa  alisema  kuwa imethibitika kuwa chanjo ni mkakati muhimu na muafaka  katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto, hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na Taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
"Nichukue fursa hii kuwapongeza akina mama na akina baba waliowapeleka watoto wao kupata chanjo kwaani chanjo ni haki ya kila mtoto; hivyo wazazi ambao hamjawapeleka watoto wenu kupata chanjo tumieni fursa hii ya wiki ya chanjo kuhakikisha watoto wanapata chanjo wanazostahili"
Alitaka  kila mkazi wa  mkoa huo kuona  wajibu  wa kuhakikisha  mtoto wake, mtoto wa jirani  au  mtoto yeyote yule anapewa chanjo ili kumzuia asipatwe na maradhi  na asiwe hatari kwa wengine.

Akitoa taarifa  ya chanjo  mkoa  wa Iringa ,mratibu  wa  elimu za chanjo  mkoa  wa Iringa  Naftari Mwalongo kuwa mkoa kwa mwaka 2016 umeendelea kutekeleza malengo mbalimbali ya Millenia yanayohusu afya likiwemo lengo namba nne(4) la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano ifikapo mwaka 2020, huduma za chanjo ikiwa ni afua mojawapo


Kuwa  katika  utekelezaji wa huduma za Chanjo kwa mwaka 2016 mkoa ulikuwa jumla ya vituo vya kutolea Huduma za afya vipatavyo  (248). Vituo vya huduma  vipatavyo (215) ambavyo ni sawa na asilimia 87 vilikuwa na majokofu na kutoa huduma za  chanjo wakati vituo vya huduma za Afya   (33) sawa na asilimia 13  vilifikiwa kwa njia ya huduma za mkoba.

 Lengo ni  kuhakikisha  huduma hizi muhimu zinasogezwa karibu na jamii  kwa kuhakikisha  kuwa kila kituo cha  kutolea huduma   za Afya kina kuwa na jokofu  na huduma za chanjo zinatolewa kila siku.


Pamoja na mafanikio haya makubwa, bado kulikuwa na changamoto ya watoto ambao hawakuwa wamekamilisha ratiba ya chanjo kulingana na umri wao.

Kuwa takwimu za mwaka 2016 zinaonesha  kuwa asilimia  6 sawa na watoto  (2,243) hawakukamilisha chanjo ya kuzuia ugonjwa   wa  Donda Koo, Kifaduro, Pepopunda, Homa ya Ini , Homa ya Uti wa Mgongo na ugonjwa wa Kupooza.

Kwa upande wa chanjo ya Surua dozi ya kwanza,  takwimu zinaonesha kuwa watoto wapatao  ( 1,495)  sawa na asilimia  nne (4) hawakupata chanjo    wakati watoto   (5,979) sawa na asilimia kumi na sita (16)  hawakupa dozi ya pili   kukamilisha chanjo ya Surua.      
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE