April 6, 2017

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR ASEMA KUSHAMIRI KWA BANDARI BUBU NI KIKWAZO KATIKA MAPATO

Na Masanja Mabula -Pemba
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed amesema, kushamiri kwa bandari bubu ni kikwazo katika ukusanyaji wa mapato na kupelekea kukodhoofisha  uchumi wa nchi.
Alisema kuwa, licha ya kuongezeka kwa mapato kwa sasa lakini pia hali ya ukusanyaji wa mapato kwa upande wa Pemba halijafikia lengo lililokusudiwa, ambapo mikakati ya Serikali ni kukusanya bilioni 800 ifikapo 2020.
Aliyasema hayo wakati alipokua akizungumza na maafisa pamoja na wafanyakazi wa TRA na ZRB, katika ukumbi wa Maktaba Chake chake Kisiwani Pemba.
“Katika mwaka 2015 tumekusanya bilioni 18 lakini kwa sasa tumeongeza hali ya mapato tumeweza kukusanya bilioni 50, hii inaonesha bado ipo fursa ya kukusanya bilioni 67 kwa mezi, makusanyo mengi hayakusanywi tubadilike wafanya kazi ili tufikie lengo tunalolitaka”, alisema.
Aidha alisema kuna mtindo ambao umeanzishwa kwa makontena kufunguliwa Mombasa na badala yake bidhaa kusafirishwa kwa majahazi kupitia bandari bubu kuingia Pemba, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti maeneo hayo ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Nae Mdhamini Wizara ya Fedha Pemba Ibrahim Saleh Juma alisema, kwa kushirikiana na watendaji wenzake watahakikisha wanahamia katika bandari bubu zilizopo Pemba, na kuziondoa mara moja ili kuhakikisha mapato yanaongezeka kwa kila hali.
“Kwa kushirikiana na watendaji wenzangu naahidi kulishuhulikia suala hili la ukusanyaji wa mapato na hatutomvumilia yoyote ambae atakwepesha ulipaji wa kodi” alisema.
Hata hivyo aliahidi kuengeza kasi katika utendaji wa kazi ili mapato yapatikane kama ambavyo Serikali imejipangilia na kuona mapato yanaongezeka kwa hali ya juu.
Kwa upande wake Mdhamini wa TRA Pemba Habibu Saleh Sultan, aliomba kupatiwa taarifa kwa bidhaa ambazo huingizwa kimagendo kutoka Mombasa na kuingizwa katika bandari bubu Pemba ili waweze kudhibiti hali hiyoWAZIRI

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE