April 9, 2017

WAWEKEZAJI KARIBU KILOLO TUINUE UTALII HIFADHI YA UDZUNGWA -DC ASIA


Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kulia akiwa na mwongoza watalii hifadhi ya Taifa ya udzungwa wakianza Safari ya kupanda mlima Udzungwa
........................................
NA MATUKIODAIMABLOG

Milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, mkoani Morogoro, wilaya ya Kilomber pia zaidi ya asilimia 40 Hifadhi hii ipo wilaya ya Kilolo ila ukosefu wa miundo mbinu umepelekea hifadhi hii kujulikana zaidi Upande wa Morogoro.

 Jitihada za serikali ya wilaya ya Kilolo chini ya mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdalah na uongozi wa mkoa wa Iringa kupitia kwa mkuu wa mkoa Amina Masenza na kamati nzima ya utalii ni kuona hifadhi za mkoa wa Iringa ikiwemo Udzungwa zinajulikana na ndio maana ya kufunguliwa kwa lango la utalii wa kusini.

Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi lakini pia ubora wa barabara hifadhi hii ni jirani zaidi kuifikia iwapo utaingilia upande wa Lilli mkoani Iringa kwani hata idadi ya wanyama ni wengi zaidi Upande wa Iringa ila kwa utalii wa kutembea kwa miguu kuona maporomoko ya maji sanje ni upande wa Morogoro zaidi.

 Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya Wadzungwa, tawi la Wahehe). Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.

 Kati ya aina kumi na moja za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni:

"Mbega Mwekundu wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979.

Mkuu wa wilaya ya kilolo na watalii wengine wa ndani ya Kilolo wakitembelea hifadhi ya Udzungwa
Safari ya utalii hifadhi ya Udzungwa
Kuna aina nyingine nne za ndege ambao hawakufanyiwa uchunguzi ambao ni: chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya aina ya kwale wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika. Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.

 "African violet" ni ua ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30. Pia Mto Sanje ni kivutio kikubwa sana Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa
mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.

 Kilolo na mkoa wa Iringa iboreshewe miundo mbinu ili kuvutia wawekezaji kujenga Hoteli za kitalii ambazo zitavutia watalii kugeukia kutembelea Udzungwa upande wa  Kilolo Iringa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE