April 11, 2017

WATANZANIA WANAOISHI NJE WAUJADILI UCHUMI WA TANZANIA


A
 Mkurugenzi wa Ikolo Investment Ltd Magidd Mjengwa akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora Tanzania Mwinyimkuu Khatibu.
A 1
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora Tanzania Mwinyimkuu Khatibu akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kushoto ni Mkurugenzi wa Ikolo Investment Ltd Magidd Mjengwa
A 2
Msanii marufu wa Kundi la Orijino Komedi Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akielezea jambo wakati wa Kongamano la Diaspora akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Magidd Mjengwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora Tanzania, Mwinyimkuu Khatibu (kushoto). Kongamano hilo la siku mbili pia linatumika kuadhimisha miaka 10 ya Mjengwa Blog iliyoanzishwa mnamo tarehe 19, Septemba, 2006.
A 3
Mtanzania anayeishi nchini Denmark Bi. Edith Chenga akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili linafanyika katika Ukumbu wa Makumbusho ya Taifa linatarajiwa kumalizika kesho tarehe 12 Aprili 2017.
A 4
Msanii marufu wa Kundi la Orijino Komedi Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamano la Diaspora lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili nafasi ya Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania.
A 5
 Mjasiriamali wa bidhaa za Dagaa Fresh wa kutoka Ziwa Victoria ambaye pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Winlab Bi. Winfrida Simo Tlatlaa akielezea baadhi ya washiriki wa Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
A 6
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akijisajili kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
A 8
Baadhi ya wawasilisha mada wakiendelea na majadiliano wakati wa Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi ya  Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania katika Kongamano lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE