April 13, 2017

WAPO WANAOTAKA KUMTEKA LEMA,KAWAPA UJUMBE HUU

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Dodoma, Lema amedai kuwa yeye haogopi vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake isipokuwa Mungu pekee.

“Ninawaonya watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake na najua uwezo wake,” alisema Lema.

“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,” aliongeza Mbunge huyo.

Kauli hiyo ya Lema imekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeeleza jana Bungeni kuwa alionywa na baadhi wa watu wakiwemo mawaziri kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge kumi na moja walio kwenye mpango wa kutekwa na genge la watu wasiojulikana.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE