April 13, 2017

UTEUZI MWINGINE ULIOFANYWA NA SERIKALI

tanzania
Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.
Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.
Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-
  1. John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
  2. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  3. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
  4. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  5. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE