April 13, 2017

UTENDAJI KAZI WA MAGUFULI WAPONGEZWA, VIONGOZI WA DINI NA WAZEE IRINGA WATOA TATHIMINI KWA MAKAMU WA RAIS

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa akieleza imani ya chama kwa serikali Mbele ya makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katikati akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza, waziri wa mazingira na Muungano January Makamba na katibu wa itikadi na uenezi
baadhi ya wafanyabiashara mkoani Iringa wakiwa Katika chakula cha pamoja na makamu wa Rais kutoka kushoto ni kutoka kampuni ya MT, Foad Abri toka maziwa ya Asas meneja TRA na mkurugenzi wa RDO Fidelis Filipatali 
Akiyekuwa mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza kushoto akiwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Iringa, Asia Abdalaha wa kilolo, Richard Kasesela wa Iringa na Jamhuri Wiliam 
Baadhi ya kinamama walioshiriki hafla ya chakula cha pamoja na Makamu wa Rais 
Na Matukiodaimablog 
WAWAKILISHI wa makundi mbali mbali ya kijamii likiwemo la wasomi wa vyuo vikuu, wafanyabiashara wazee  na viongozi wa dini mkoani Iringa wamepongeza utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuwa kazi inayofanya ni zuri na inapaswa kusonga mbele zaidi isisikilize wanaolalamika kwa kubanwa kufanya ufisadi.

Wakizungumza jana wakati wa chakula cha pamoja na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alichokiandaa katika Hoteli ya NSSF kwa wawakilishi wa makundi yote mkoani Iringa,walisema kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano ni ya kupongezwa. 

Mkuu wa chuo kikuu cha Iringa Profesa Joshua Madumla alisema kazi inayofanywa na serikali ya Magufuli inaonekana na inawanufaisha wananchi wote 

Hivyo alisema Rais asikubalu kurudishwa nyuma kuwatumikia watanzania kutokana na mameno ya wachache wasiopenda kuona watanzania wananufaika na raslimali za Taifa hili kwani alisema hakuna asiyejivunia utendaji kazi mzuri wa Rais na serikali yake. 

Japo aliomba serikaki ya Rais Magufuli kwa wana Iringa kusaidia kuboresha kwa kiwango cha lami barabara ya Ipogolo kwenda wilaya ya Kilolo ambayo ni barabara ya kiuchumi pamoja na ile ya Iringa kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha. 

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas  ,Found Abri alisema wao kama wafantabiashara wanapongeza serikali kwa usikivu mkubwa na kipekee wanamoongeza Rais na makamu huyo wa Rais ambao wamekuwa wakisikiliza kilio chao. 

Hata hivyo aliomba serikali kuendelea na usikivu huo na pale kwenye changamoto kati yao basi kutosita kuifanyia kazi huku akipongeza urendaji wa meneja wa TRA mkoa wa Iringa. 

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro alisema kuwa watanzania wanajivunia utendaji kazi wa Magufuli na wanatembea kifua mbele na kuwa anayesema vibaya juu ya serikali si mzalendo na anayake mambo. 

kandoro aliomba serikali kama ilivyoanza kuonyesha jitihada za kunusuru mto Ruaha mkuu kuendelea kufanya hivyo ili mto huo kudumu zaidi. 

Mbunge mstaafu wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu pamoja na kuipongeza serikali bado aliomba kusaidia kupambana na matukio ya ubakaji mkoani hapa na kumwomba makamu wa Rais atakaporudi kwa ziara ya kikazi mkoa wa Iringa kukaa na wanawake wa mkoa huo. 

Mwenyekiti wa waganga wa tiba asilia mkoa wa Iringa Christina Mgongolwa alisema kuwa wao wanapongeza serikali kwa kazi nzuri na kuwa isisite kuwa karibu na waganga hao Kwani mambo ya kukauka kwa mto Ruaha ni kutokana na watu kupuuza mila na wapo tayari kurejesha mila iwapo serikali itaendelea kuwajali. 

Huku viongozi wa dini mbali mbali akiwemo askofu mstaafu wa Anglikana Tanzania Dolnad Mtetemela wakidai kuwa serikali ya Magufuli imewakuna kwa utendaji kazi na wapo tayari kushirikiana na kutaka isirudi nyuma. 

Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia alipongeza kwa maoni ya wanchi hao na kuwa atafanya ziara ya kikazi mkoa wa Iringa mwezi ujao na kuwa atakuja na majibu ya maoni hayo huku akisema suala la ubakaji katika mkoa wa Iringa bado mkoa unalimudu japo Taifa litaingiza nguvu yake. 

Pia kuhusu barabara ya lami kilolo na Iringa kwenda hifadhi ya Taifa alisema inawezekana. 

Akitoa maoni yake mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho mkurugenzi wa taasisi ya RDO  kutoka wilaya ya Mufindi Fidelis Filipatali alisema utaratibu huo wa makamu wa Rais kukutana na makundi mbali mbali mkoani ni mzuri na unaonyesha jinsi gani serikali ilivyosikivu na inayojishusha kwa wananchi wake.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE