April 11, 2017

UGONJWA WA AJABU WAMTESA MTOTO HUYU IRINGA MJINI, ALAZIMIKA KUACHA SHULE AKISUBIRI MAAMUZI YA MUNGU

mtoto Ayubu anayesumbuliwa na uvimbe akiwa na mamake mdogo 
Mtoto Ayubu Akisaidiwa kuvua shati 


Mtoto Ayubu akiwa nje ya nyumba yao. 
Na Matukiodaimablog 


MATESA na mahangaiko anayopata mtoto Ayubu Chengula (9) mkazi wa Kigamboni katika kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa mkoani Iringa yapelekea familia yake kukata tamaa ya kuendelea kumuuguza baada ya kuzunguka Hospitali mbali mbali bila kupata majibu ya tatizo lake.

" Tumepata kumpelea Hospitali mbali mbali kama Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,Ikonda wilaya ya Makete mkoa wa Njembe na tumefika hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kila wakipima hakuna jibu wanalolipata tumepima hadi kansa ila hakuna kituo hivi sasa tumekata tamaa tunasubiri huruma ya watanzania ili kuweza kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu "alisema mama mdogo wa mtoto huyo .

Akizungumza na mwandishi wetu mkoani Iringa mama mdogo wa mtoto Ayubu Scolla Nyigo alisema kuwa baba na mama wa mtoto huyo ni wakulima wakazi wa Tanangozi Halmashauri ya Iringa vijijini ambao wamezunguka na mtoto huyo maeneo mbali mbali kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa bila kufanikisha matibabu yake .
Hivyo kwa sasa wazazi hao kama wamekata tamaa kuendelea kuzunguka na mtoto wao huyo kwenye matibabu na ndio sababu ya kumleta mjini Iringa kwa ajili ya kuendelea kupumzika akisubiri maamuzi ya mwenyezi Mungu dhidi yake hapa duniani .

" Kweli kama kuzunguka tumezunguka kila kona ya nchi hii kutafuta matibabu ya mtoto wetu hadi hapa tulipo hatuna pesa ya kuendelea kuzunguka kutafuta matibabu hivyo mgonjwa yupo tu hapa nyumbani hasomi wala hafanyi kazi yeyote yeye ni kula na kulala tu "

Alisema eneo ambalo wanaishi ni jirani na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ila hawajabahatika kwenda Ofisini kweke kwa ajili ya kuomba kusaidiwa kutafutiwa wasamaria wema kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto huyo ila wanaomba ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa ama ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na wafanyabiashara wa mjini Iringa kuweza kusaidia matibabu ya mtoto huyo.

" Tumechanganyikiwa na ugonjwa wa mtoto huyu ulianza kama muwasho mwilini katika mkono wake wa kulia tatizo ambalo lilimuanza akiwa darasani na wenzake akiendelea kujisomea na kutokana na uvimbe huo kuendelea kukua siku hadi siku alilazimika kukatisha masomo mwaka jana akiwa darasa la pili ili kuendelea kuugulia nyumbani tatizo hilo .

Thimotheo Mwagange ni jirani wa kijana huyo alisema kuwa baada ya kuona tatizo la mtoto huyo linazidi kukua siku hadi siku kwa upande wake aliendelea kumpa huduma ya maombi kulingana na uwezo wake wa kitumishi huku akitafuta njia ya kuonana na mwandishi wa habari wa matukiodaima  kwa ajili ya kuomba msaada zaidi wa kuhabarisha umma ili kusaidia kunusuru maisha ya mtoto huyo .

Iwapo upo mkoani Iringa unahitaji kufika kumtembelea kumjulia hali ama kumsaidia mtoto huyo wasiliana na mwandishi na mmiliki wa mtandao huu wa matukiodaima   Francis Godwin kwa namba 0754 026299 ili kuweza kukuwezesha kumfikia mtoto huyo kwa maoni ya kunusuru uhai wake. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE