April 28, 2017

TUNAENDELEA KUMSHIKILIA DKT JESCA MSAMBATAVANGU - POLISI

RPC  Iringa  Julius Mjengi
                                                                Dkt  Jesca  Msambatavangu

ZIKIWA zimepita siku  moja   toka  aliyekuwa mwenyekiti  wa chama  cha mapinduzi (CCM) aliyefukuzwa uanachama  na chama  hicho  Dkt  Jesca  Msambatavangu  kushikiliwa na  jeshi la  polisi kwa  tuhuma  za kuratibu tukio la  kumfanyia vitendo vya  kinyama  mwanamke  mmoja  mkazi  wa Kibwabwa katika  Manispaa ya Iringa ,jeshi la  polisi limesema  linaendelea kumshikilia kwa  upelelezi  wa tukio  hilo.

Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi  amezungumza na mtandao wa matukiodaimaBlog  kuwa Msambatavangu  atafikishwa  mahakamani kujibu  tuhuma  zake pindi  upelelezi  wa shauri hilo  kukamilika .

Alisema  kuwa  bado  jeshi lake  linaendelea  kuwasaka watuhumiwa  wenzake  watatu  walioshikili katika tukio  hilo la  kumfanyia vitendo  vya  kikatili mwanamke  huyo ikiwa ni  pamoja na kumchoma  sindano  inayosadikika  kuwa na  sumu .

Hata  hivyo  alisema  tayari  wanayomajina ya  watuhumiwa hao  watatu  waliotajwa  kuhusika na  tukio  hilo na msako  unaendelea  ili  kuwakamata  .
 
Aidha  alisema  kuwa mwanamke  huyo  yupo  katika mazingira  salama na  hawezi  kupata  madhara yoyote kwani  jeshi  lipo kwa ajili ya  ulinzi wa raia na mali  zake huku  akidai kuwa  sababu za  kiusalama vimepelekea kutotaja  majina ya  wanaotafuta na jina  hali la mwanamke  huyo kwa  usalama  wake .

Imeelezwa  kuwa  chanzo  cha  mwanamke  huyo kufanyiwa vitendo  hivyo  vya ukatili  ni  kutokana  visa vya  kisiasa kati ya  aliyekuwa mwenyekiti  wa CCM mkoa na mwanamke  huyo ambae alionyesha  kufurahia hatua ya mwenyekiti  huyo  na  wenzake  wasaliti ndani ya  CCM kufukuzwa chama.

Kwani  mwanamke   huyo  ambae pia ni kada  wa  CCM imeelezwa  hata  wakati wa mchakato  wa  kura  za maoni ndani ya  CCM kwa  ajili ya  kumpata mgombea ubunge wa CCM jimbo la  Iringa mjini nafasi  ambayo iliombwa na  wanachama  zaidi ya  6  akiwemo Dkt  Msambatavangu  hakuwa upande  wake .

Dkt  Msambatavangu ambae baada ya  kufukuzwa chama amekuwa  akisimamia  shughuli  zake  mbali mbali  zikiwemo za  Kilimo ,shule  zake,duka  la  kubadili pesa na shughuli za  dini kukamatwa  kwake  kumepokelewa  kwa  hisia tofauti  mkoani Iringa na katika mitandao  ya  kijamii  kwa  watu kuwa na maoni  tofauti  juu ya suala hilo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE