April 13, 2017

Tuianze siku kwa Maombi.

... 

baba Mungu mwingi wa 
Huruma asubuhi hii kwa unyenyekevu Mwingi tunasema ahsante amini tumeuona ukuu wako. 

Tunaomba tushike mkono utufinyange kwa mkono wako 
na tufanye vile utakavyo Mungu kwani tunaona faida ya kukutumaini wewe kamwe hatutikiswi na adui shetani. 

Jina lako Mungu lapita majina yote kwani wewe umponyaji wetu hivyo twaomba waponye wote wagonjwa na kupitia jina lako Mungu tunaomba tukuite dereva wetu kwa wote tunao safiri na tukuite mfariji kwa wafiwa. 

Tunakili ushindi wetu kupitia wakolinto wa kwanza kuwa lakini Mungu ashukuliwe atupaye kushinda, nasi twakutumaini wewe kuwa tu washindi pamoja nawe. 

kipekee asubuhi hii Mungu ombi letu kubwa kwako ni kuliombea Taifa letu kuondokana na matukio ya ukatili mbali mbali hasa tukiomba wafichue na kuwaadhibu wale wote wanaojihusisha vitendo vya ubakaji na ulawiti twasema hawana mamlaka ktk Taifa hili na tunakemea kwa nguvu zote Mungu matukio haya. 

Mungu amini roho zetu zachukizwa na dhambi na maasi haya hivyo tunaomba sema nasi na tuepushe Mungu 

AMEN

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE