April 12, 2017

TUIANZE SIKU NA MUNGU...Mbele zako Mungu twanyenyekea na kuomba kwani sisi si wasafi wa kujisifu hata kushindwa kuomba msamaha wako pale tulipo kosea

Hivyo Mungu twasema ahsante kwa ulinzi wako na msamaha wako ni tiba ktk maisha yetu asubuhi hii tunaomba ulinzi wako popote tutakapo kwa tushinde nawe na tuepushe na adui shetani.

Tunaomba Mungu kipekee bariki nchi yetu na wawakilishi wetu bungeni ambao kwa sasa wamejawa na hofu ya matukio mbali mbali yanayotokea hapa nchini kama utekaji na mengine Mungu tunaomba uwe mlinzi wa Taifa letu kwani wewe pekee ndio tegemeo na mlinzi wa kweli.

Mungu tunaomba baraka tele kwa nchi yetu pia viongozi wote wa Taifa hili uwabariki Mungu wape afya njema.


Wagonjwa ukawaponye, wafiwa ukawafariji na wenye shida mbalimbali ukawe mtatuzi wa shida zao na wasafiri ukawaongozi

Kwako Mungu wetu twaomba na kuamini

Amen

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE