April 26, 2017

TEHRAN KUSAIDIA FILAMU ZA TANZANIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo tarehe 25 Aprili, 2017 ametembelewa na Balozi wa Iran nchini, Mhe. Mousa Farhang kwenye ofisi ya Wizara, Dodoma. Katika maongezi yao Mhe. Balozi ameishukuru Serikali kwa kuendeleza ushirikiano wa karibu na nchi ya Iran kwenye maeneo ya Sanaa na Utamaduni hususani kwenye maonesho ya wiki ya utamaduni ya Shiraz yaliyofanyika takribani miezi mitatu iliyopita Dar es Salaam na Zanzibar. 
Maonesho hayo yaliwakutanisha pamoja wananchi kutoka Iran na Tanzania. 

Aidha, Mhe. Balozi alitumia nafasi hiyo kutoa mwaliko kwa Tanzania kushiriki kwenye maonesho kama hayo ya wiki ya utamaduni wa Shiraz yatakayofanyika tena nchini Iran mwaka huu. Mhe. Balozi wa Iran pia amemuahidi Mhe.Waziri kusaidia na kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya filamu na sanaa kwa ujumla.

 Kwa upande wake Mhe. Mwakyembe alimshukuru Mhe. Balozi kwa kumtembelea Wizarani na alimhakikishia ushirikiano na urafiki katika masuala ya Sanaa na Utamaduni. Mhe. Mwakyembe alimuahidi Mhe. Balozi kwamba Serikali itawasisitiza wasanii wa ngoma na filamu nchini kutumia fursa zitakazotolewa na Serikali ya Iran na hivyo kuwawezesha kujifunza tamaduni zilizopo na kujiendeleza kwenye tasnia ya filamu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE