April 22, 2017

TAZAMA MBIO ZA MAGARI ZA MAJI MKWAWA ZILIVYOTIKISA MJINI IRINGA

Mshiriki  wa mbio  za magari  mkoa  wa Iringa  Ahmed Huwel  ambaye ni mdhamini wa mashindano hayo  kupitia kiwanda kipya cha maji Mkwawa akionyesha ujuzi wake  wa kucheza na gari  wakati  akiondoka  uwanja wa Samora kuanza  mbio   hizo  leo  jumla ya  washiriki20  kutoka mikoa  mbali  mbali wanashiriki mashindano hayo yanayofikia kilele  chake kesho
MASHINDANO  yam bio  za  magari  yasimamisha  shughuli  za  wakazi wa Manispaa ya Iringa   baada ya  wananchi  kufunga maduka  yao kujipanga   barabarani na wengine  kufurika uwanja wa Samora  kushuhudia  mashindano hayo leo 
Mashinmdano  hayo yalioanzia kiwanda  cha maji  Mkwawa na  pointi yake ya  pili  kuwa  uwanja wa  Samora  ambako umati mkubwa wa  wananchi  walifurika katika uwanja huo yameanza kwa  ushindani mkubwa kati ya  Ahmed  Huwel ambaye ni mdhamini  wa mashindano hayo kupitia kiwanda cha maji  afrika na mkulima wa Arusha Gerald  Miller .
Pamoja na  washiriki  hao  wawili  kuonyesha  mbwembwe na ushindani mkubwa  bado  mwenyekiti wa  klabu yam bio za magari  mkoa wa Iringa  Hamidu Mbata  alionyesha   kuwavuta  wengi  uwanjani hao  ambako ndipo  pointi  ya pili ilikuwepo .
Mashindano hayo yaliyoianza  leo  aprili  22 yatakimbia  kilomita 300 Ana  kesho Aprili 22  yatahitimishwa  huku   washiriki  20 ndio  wanaochuana .
Akizungumza kwa  niaba ya  mkuu  wa  mkoa wa Iringa ,mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi ,Jamhuri  Wiliam alisema  mashindano hayo ni  fursa  kubwa kwa  wana Iringa hasa katika  kuyatumia  kuongeza kipato chao kwa kupitia biashara  zao .
Mkuu  huyo  alisema burudani ambayo  wana Iringa  wameipata kupitia  mbio  hizo za magari ni burudani ambayo imepokelewa kwa  shangwe kwa wananchi wa mkoa  wa Iringa .
Huku  mkuu  wa  wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliwataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuendelea kuchukua tahadhari wakati wa mashindano hayo ya magari yanayoendelea  .
“Katika barabara zote ambazo magari hayo yatapita, tunaomba watu wasikatize kabla magari hayo hayapita lakini pia tunatoa wito kwa madereva wa bodaboda kutotumia barabara zitakazotumika wakati wa mashindano hayo,” alisema.
Kwa  mujibu  wa  ratiba  iliyotolewa na , Mwenyekiti wa Klabu ya Magari Iringa, Hammid Mbata alisema mashindano hayo yanafanyika ikiwa ni zaidi ya miaka 10 toka yafanyike kwa mara ya mwisho.
“Hapo katikati tulishindwa kuandaa mashindano hayo kwasababu ya kukosekana kwa udhamini madhubuti,” alisema.
Alisema mashindano hayo  yameleta  wageni zaidi ya 200 mjini Iringa ni kichochea cha biashara, utalii na maendeleo ya jumla ya mkoa wa Iringa.
Alisema  siku ya kwanza mashindano hayo yatapita katika kijiji cha Kigonzile, Mgongo, Igingilanyi, Kiwele na kutokea Chuo Kikuu cha Mkwawa huku siku ya pili yatapita kijiji cha Wenda, Kikombwe, Tanangozi, Kalenga, Makongati, Kiponzelo, Ifunda, Mgama na Ihemi. 
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Steven Nyandongo alisema katika njia ambazo mashindano hayo yatapita kuna maeneo hatarishi yatakayodhibitiwa kwa usalama.


Mshiriki  wa mbio  za magari  mkoa  wa Iringa  Ahmed Huwel  ambaye ni mdhamini wa mashindano hayo  kupitia kiwanda kipya cha maji Mkwawa akijiandaa kuonyesha ujuzi wake  wa kucheza na gari  wakati  akiondoka  uwanja wa Samora kuanza  mbio   hizo  leo  jumla ya  washiriki20  kutoka mikoa  mbali  mbali wanashiriki mashindano hayo yanayofikia kilele  chake kesho
wananchi wa mji wa Iringa  wakiwa kando ya  barabara  kushuhudia  mbio za  magari

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE