April 15, 2017

TANESCO IRINGA YAWAKUMBUKA YATIMA CHAKULA CHA PASAKA

Mwenyekiti  wa  chama cha wafanyakazi TUICO tawi la Tanesco  mkoa wa Iringa  Jeremia Mwakipesile  kushoto  akikabidhi msaada  wa  vyakula na  vitu mbali mbali kwa  watoto yatima wa  kituo cha Ruhuma  Center kwa  niaba ya  wafanakazi wenzake   waliotoa kwa  ajili ya  sikukuu ya  Pasaka  kwa  yatima hao leo
Baadhi ya  wafanyakazi wa  TANESCO  Iringa  wakiwa kituoni hapo
Wafanyakazi wa  TANESCO  wakisogeza  msaada  wao
Yatima na mlezi wa  kituo wakipokea  msaada wa  vitu mbali mbali
Mwenyekiti wa  wafanyakazi  Tanesco Iringa Jeremia Mwakipesile  kushoto akikabidhi msaada wa chakula kwa  yatima
Baadhi ya wafanakazi wa Tanesco  wakisikiliza maelezo ya  kituo
Mwenyekiti wa wafanyakazi  Bw Mwakipesile  akitoa taarifa ya  msaada huo
Wafanyakazi wa Tanesco  wakimsikiliza mwenyekiti  wao
Baadhi ya  yatima  kituoni hapo
Mfanyakazi wa Tanesco Iringa  akiwa na mtoto yatima
WAKATI  kesho  wakristo   kote  ulimwenguni wanaungana  kusherekea  sikukuu ya  kumbukumbu ya kufufuka kwa  Yesu  Kristo , watumishi  wa  shirika la umeme  Tanzania (Tanesco)  mkoa  wa Iringa limetoa msaada  wa  chakula kwa  ajili ya watoto  yatima  wa  kituo cha Huruma Center kilichopo mjini Iringa .

Akikabidhi msaada  huo  leo  kwa  niaba ya  wafanakazi  wengine mwenyekiti  wa chama  cha  wafanyakazi (TUICO) Tanesco Iringa Jeremia Mwakipesile  alisema  kuwa  imekuwa  ni kawaida ya  wafanyakazi  hao  kukumuka watoto yatima  na  wajane  wakati wa sikukuu  mbali mbali kama sehemu ya  kuwaikumbusha jamii  kuwajali  watu  hao  wenye  shida.

“ Sisi kama  wafanyakazi wa Tanesco  mkoa  wa  Iringa  imekuwa ni kawaida  yetu kuwasaidia yatima  na  watu wenye  sihida mwaka jana tumetoa msaada  kwa  yatima na  walemavu Ilula  wilaya ya   Kilolo na  tumekuwa tukifanya hivyo  kila  inapohitajika”

Alisema   kuwa  wamevutiwa na  malezi  bora ya  kituo  hicho  cha  Ruhuma Center kwa kazi nzuri ya  kujitolea  kuwasaidia  watoto hao na kuwaomba  kuendelea na  moyo wa  kujitolea .

Mwakipesile  alisema  kuwa bado jamii  inapaswa  kuendelea  kujirtolea   kusaidia  yatima wakati wa  sikukuu  badala ya  kuzijali familia  zao  pekee na  kuwa  wao  wamelazimika  kutoa vituo mbali mbali kama  mchele  kilo 50 ,mafuta  ya  kula , sabuni ,nguo ,maharage na mahitaji mengine  madogo madogo kwa  ajili ya  watoto hao kufurahia  sikukuu .

Wakati  mwakilishi  wa  meneja  wa  Tanesco  mkoa wa Iringa Sembe  Hoteli alisema  kuwa  shirika la Tanesco pamoja na mambo mengine   ya  utoaji wa  huduma ya  umeme bado  shirika  halitaacha  kusaidia jamii inayowazunguka .

Mlezi  wa  kituo  hicho mchungaji Joyce  Ngweta  pamoja na  kushuruku msaada  huo  alisema kuwa   kituo  hicho kipo  chini ya kanisa la Kiinjili la  kilutheri  Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa  kilianzishwa  mwaka  1994 kina  watoto zaidi ya  40 .

Aidha  alisema kuwa  kituo  hicho kinaendelea  kutunza  watoto   nje ya  kituo  kwa  kuwapa  huduma   huko huko na  kuwa  watoto  11  hivi  sasa  wanatunzwa  majumbani  na wanaendelea na elimu ya  sekondari  na kufanya jumla ya  watoto  wote  kufikia 51.

Akielezea  kuhusua  changamoto  mbali  mbali  zinazokikabili  kituo hicho  alisema  ni pamoja na  baadhi ya  wahisani  kusitisha kutoa msaada kwa  kituo  pamoja na  ile ya  jamii  kufarakana katika  ndoa na  kupelekea  watoto  kukosa malezi  mazuri .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE