April 8, 2017

TAIFA TUJINYENYEKEZE MBELE ZA MUNGU KWA MAOMBI...Tuna kushukuru mwenyenzi Mungu kwa Rehema zako umetuamsha salama .

Nasi hatuchoki kukuabudu wewe maana sisi ni wahitaji siku zote na jina lako ni ulinzi kwetu.

Tunazidi kutafakari neno lako kwani latubariki na hatutaki kufananishwa na neno ktk zaburi 14:1-3
 Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu wameharibu matendo yao na kufanya chukizo hakuna atendae mema

Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu aone kama yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu ,wote wamepotoka wameoza pamoja hakuna atendaye mema la !hata mmoja

Bwana si hivyo twatambua si Kwa uwezo wetu ni kwa uwezo wako tupo hai na tupo kukuomba hekima yako asubuhi hii tembea nasi Kazini, safarini, na hata mahospitalini ukawaponye wagonjwa iwapo wapo katikati yetu ktk katika kundi wanaumwa ama kuuguza Mungu kwa damu ya mwanao Yesu kristo shusha uponyaji,wasafiri ukawe dereva wao, wafiwa ukawafute machozi.

Mungu tunaomba onekana kwenye shughuli zetu zote leo  wewe ukawe nasi maana tupo kwenye maandalizi ya Pasaka na changamoto za kukusifu wewe ama tutavaa nini na kula nini zisiwe kikwazo ktk familia zetu maana Wewe ni Mungu mwenye nguvu na kila aombae kwa jina lako hupewa.

Tunaliombea Taifa letu Amani izidi mauwaji ya raia wasio na hatia pale Rufiji sasa iwe basi, utekaji uliofanyika kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake iwe mwisho na kwa kuwa nguvu na ulinzi wako wazidi ulinzi wowote hapa Duniani Mungu tunaomba tenda miujiza yako rejesha furaha kwenye familia za watu hao na watanzania wengi twataka kuwaona ndugu zetu tunaomba nyosha mkono wako sasa kuwashika na kuwafichua ndugu zetu.

Tunakemea kwa nguvu zote uonevu na maasi ya kila aina kwenye taifa letu mpe afya njema Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli azidi kututumikia vema pia tunawaombea viongozi wetu Mungu afya njema.

Tusikie Mungu katika maombi yetu tubariki sote na familia zetu zoteAMEN.....

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE