April 18, 2017

SIWEZI KUDANGANYA WANANCHI KWA KUSIFIA KILA JAMBO , HALMASHAURI YA IRINGA NIPENI BOQ YA JENGO HILI AU TUKUTANE MAHAKAMANI .

 

baadhi ya mbao za fishabody katika jengo la Halmashauri ya Iringa DC zikiwa mbioni kudondoka kutokana na uchakavu japo jengo hilo lina wapangaji na kila mlango hutozwa kati 350000  ila hali ya jengo ndio hivyo tena 

LEO kama mkurugenzi  wa mtandao  wa matukio daima imefarijika kupokea barua  kutoka kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa mkoani  Iringa awali  nilijua ni barua ya  mwaliko wa mbio  za mwenge  ili  kuwasaidia  kusifia miradi yao .

Lakini  barua   hii kweli   wacha  nisimalizie  kusoma kwani  nikiendelea  moyo wangu una majonzi kilichoandikwa  sijakitambua eti nikanushe  ukweli  kuweka uongo hapana  mimi  sipo  hivyo  nipo kusema  ukweli zaidi na  nilichoandika ni mtazamo  wangu na hakuna wa kunifundisha   kuwaza kama yeye hii ni ndoto nani anayenipa maagizo  niote  ndoto kama  yake?

Ni ukweli kuwa  katika  tasnia ya habari lazima  kuzingatia maadili kwa  kuhoji upande wa pili  ila  kwa picha hii ya jengo kuanza  kubomoka nani anisaidie  kutazama ? leo  wamekwenda  kukarabati ndipo  wananiambia  nikanushe hivi kweli Halmashauri ya  Iringa inayoongozwa na mkurugenzi  Msomi  inaruhusu watu  waandike  barua   za  vitisho kama  hivi badala ya  kushukuru  kwa taarifa  inatoa  vitisho ?

Kwanza  nawashukuru  kwa kuwa  wasomaji  wazuri wa mtandao wa matukiodaimaBlog ila naomba  sana tusitishane tutaogopa  kuendelea  kuibua kero za  wananchi hivi ni nani  asiyejua kuwa  Halmahauri ya manispaa ya  Iringa ambako mmewekeza ujenzi wa jengo la  biashara lenu  ilizuia ujenzi wa majengo ya aina ya kwenu na kutaka  wananchi  kujenga maghorofa  ni nani aliyevunja  sheria pia  ninyi  mnaona  mlichokifanya ni  wasa  kujenga  jengo hilo badala ya  ghorofa  eneo zuri kama  hilo ila  BOQ yenye  ilisemaje na mmefanya  nini acheni  kutisha  watu .

 Kwenye  barua ya  kutaka  kukanusha mmenitaka  nikanushe kwa  jengo  hili halijajengwa kwa milioni 400 ila hamjasema limejengwa kwa pesa  ngapi na BOQ  yake hamjanipa hamuoni kuwa  kukanusha   ni kupotosha zaidi naomba  hizi  siku 14  mlizonipa kukanusha  nipeni ushirikiano wa  kunipa BOQ pia sababu ya  jengo hili kuanza  kuharibika  ndani ya muda mfupi na ikipendeza mkandarasi aliyejenga lakini  pia matumizi ya  jengo hili yanatumiza  ilivyo .

 Mkurugenzi wa  Halmashauri Robert Masunya najua  wakati  huo  haukuwa mkurugenzi Iringa usikubali  kupotoshwa tafuta  BOQ na chukua hatua  ya  kuwawajibisha hawa wanaotaka kuharibu kazi yako  pia maofisa habari  wako waende kwa wananchi  wasiende kwa  waandishi kutafuta  waandishi  wanaoisaidia Halmashauri .

Ndani ya  siku 14  nilizopewa  nitaandika  habari  za wananchi wa Halmashauri ya  Iringa bila  kumuogopa  mtu kesho nitaleta  taarifa ya masoko ya yaliyojengwa kwa  mamilioni ya  shilingi ila  hayatumiki hakuna  shida heri kusema ukweli na kuwa na maadui  kuliko  kusifiwa naliamsha  Dube nasema  Halmashauri ya Iringa tukutane Mahakamani .

 JENGO HILI LA HALMASHAURI YA IRINGA NI JIPU


Mkazi wa Manispaa ya Iringa akipita kando ya jengo la Halmashauri ya Iringa ujenzi wake umekuwa ukinyoshewa vidole kutokana na ujenzi wa jengo hilo ambalo lilikamilika mwaka 2011 ila kutokana na kuwepo kwa kijiharufu cha ufisadi hadi leo hakuna jiwe la msingi wala uzinduzi au kiongozi yeyote kuonyeshwa au kutembelea mradi huu ulioteketeza zaidi ya Tsh milioni 400 za walipa kodi japo BOQ yake ilikuwa ni kujengwa ghorofa nitaendelea kufukua makaburi 
Mkazi wa Manispaa ya Iringa akipita kando ya jengo la Halmashauri ya Iringa ujenzi wake umekuwa ukinyoshewa vidole kutokana na ujenzi wa jengo hilo ambalo lilikamilika mwaka 2011 ila kutokana na kuwepo kwa kijiharufu cha ufisadi hadi leo hakuna jiwe la msingi wala uzinduzi au kiongozi yeyote kuonyeshwa au kutembelea mradi huu unaodhaniwa kuteketeza kwa zaidi ya Tsh milioni 400 za walipa kodi japo BOQ yake ilikuwa ni kujengwa ghorofa nitaendelea kufukua makaburi 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE