April 29, 2017

SIKU YA MAKONDA DAR YAPEWA KISOGO?

maduka eneo la Sinza madukani jijini Dar, yakiwa yamefungwa leo saa 2 asubuhi kutokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salama kwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa ya usafi maarufu kama siku ya Makonda na wafanyabiashara kutofungua maduka hadi saa 3 ili kufanya usafi maeneo yao japo leo hali si hivyo kwani maduka wamefunga bila kufanya usafi maeneo yao hivyo ndio kusema siku hii imepuuzwa ama imepewa kisogo? 
Kuna haja ya viongozi kabla ya kutoa matamko mbali mbali kwanza kujifunza historia ya wakazi husika ama kuangalia utekelezaji wa agizo husika na usimamizi wake maana kinachoendelea Dar, kwa sasa si utekelezaji wa agizo bali ni upuuziaji wa agizo na kwa kuwa wafanyabiashara na wananchi wanajua ni kosa kufungua maduka kabla ya saa 3 asubuhi kwa jumamosi ya mwisho wa Mwezi wanachokifanya ni kulala hadi saa 3 na kisha kuamka kwenda kufungua shughuli zao sina hakika kama kwa mwendo huu kuna utekelezaji wa agizo la usafi nachoona mimi wameongezewa muda wa kuchelewa kuamka. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE