April 9, 2017

SIKU NJEMA NA MATENDO MAKUU YA ROMA MKATOLIKI

Tuianze jumapili hii kwa kutafakari somo toka kitabu cha Mika 3:8-12


 8 Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
 9 Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili.
 10 Wanaijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. 
11 Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea Bwana, na kusema, Je! Hayupo Bwana katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia.
 12 Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.

Tuombe........ 

Ahsante Mungu umetuamsha wenye furaha na afya njema umerejesha furaha kwa nyumba zilizokosa furaha kutoondoa hofu watanzania na dunia juu ya utekaji na uovu uliojitokeza kwa Roma Mkatoliki na wenzake, ila Mungu katika maombi yetu jana asubuhi tuliomba ndugu zetu wapatikane na wamepatikana bado Mungu shauku yeye kusogea mbele zako kwa unyenyekevu tena tuonyeshe makusudi ya watekaji hawa nawe kwa wakati wako uweze kuwalipa sawa na uovu waliotenda. 


Tunasema ahsante maana umesikia uomba kwetu, tuonaomba asubuhi hii bariki wasafiri na wote wenye shida Mungu kipekee serikali yetu na Rais wetu mpe afya njema

Kwako Mungu twaomba na kuamini 

AMEN 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE